A

A

Nani kukatwa nani kubaki???Mbowe Kufanya Mabadiliko ya Baraza Lake Mawaziri.

Na Mwandishi,

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe anatarajiwa kufanya mabadiliko ya baraza lake kivuli la mawaziri.

Katika mabadiliko hayo, Mbowe anatarajiwa kuingiza sura mpya, kuhamisha baadhi wizara, wengine kubaki kwenye nafasi zao huku akiwatoa baadhi yao.

Kwa mujibu vyanzo mbalimbali ndani ya kambi hiyo, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anatarajiwa kulitangaza baraza hilo wakati wowote.

Baraza kivuli alilolitangaza Februari 5, 2016 bungeni jijini Dodoma lilikuwa na wizara 18 likijumuisha vyama washirika wa Ukawa vyenye wabunge; NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF.

CUF kwa sasa imegawanyika katika pande mbili; upande unaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na upande wa katibu mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuzingatia ongezeko la

MAGUFULI AKABIDHIWA RIPOTI, KIFUATACHO CCM NI KUSAFISHA SAFISHA NA KUIMARISHA CHAMA

Tume ya kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyoundwa na Rais John Magufuli, imebaini madudu ukiwamo utapeli na usimamizi mbaya wa mali hizo.

Kamati hiyo iliyoundwa na Rais Magufuli kukagua mali za

NAIBU SPIKA AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WATU WASIO SIKIA


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto)

Kesi Ya Babu Tale Yaahirishwa, Arudishwa Mahabusu

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale maarufu Babu Tale, leo Mei 23, 2018 saa 6 mchana amefikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi inayomkabili, akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Babu Tale, ambaye pia ni meneja wa mwanamuziki maarufu wa

WACHEZAJI 30 KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA

Na Agnes Francis Blogu ya Jamii.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)limetangaza majina ya wachezaji 30 katika kuelekea mwisho wa Ligi  kuu  ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ambao watawania Tuzo za Mchezaji Bora mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa TFF Clifford Ndimbo amesema utaratibu huo hufanyika kila mwaka baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Vodacom.

Ndimbo amefafanua wachezaji hao 30 watachujwa na kubaki 10 na baadae watabaki wachezaji wa tatu wataoinga hatua ya fainali ili kumpata Mchezaji bora kwa msimu huu.

Amewataja wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Habibu Kyombo (Mbao),Khamis Mcha,(RuvuShooting),Yahya Zayd(Azam),Razack Abalora(Azam), Bruce  Kangwa(Azam) Aggrey Morris(Azam),Himid Mao (Azam),Awesu Awesu(Mwadui) na Adam Salamba(Lipuli).

Wengine ni Mohammed Rashid(Prisons), Shafiq Batambuze(Singida),Mudathir Yahya (Singida), Marcel Kaheza(Majimaji),Ditram Nchimbi(Njombe Mji) na Eliud Ambokile(Mbeya City).

Pia Shaaban Nditi(Mtibwa), Tafadzwa Kutinyu(Singida) Ibrahim Ajibu(Yanga), Gadiel Michael(Yanga),Papy Tshishimbi(Yanga),Kelvin Yondani(Yanga),Obrey Chirwa(Yanga),Aishi Manula(Simba), Emmanuel Okwi(Simba),John Bocco(Simba), Jonas Mkude(Simba),
Erasto Nyoni(Simba),Shiza Kichuya(Simba),Asante Kwasi(Simba),Hassan Dilunga(Mtibwa).

"Mchakato wa kupata mchezaji bora unatarajia kufanyika Juni 23 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ambapo msimu huu kutakuwa na washirika wengine Azam Tv, Benki ya KCB na Premier Bet,"amefafanua

Pia amesema licha ya tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, kutatolewa tuzo mbalimbali, ambapo kwa mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine imeongezwa ikiwa ni katika uboreshaji

"Tuzo iliyoondolewa ni ya Mchezaji Bora wa Kigeni na imefanyika hivyo ili kuwapa fursa wachezaji wote kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL badala ya kuwatenganisha, vile vilee msimu huu imeongezwa Tuzo ya Mwamuzi Bora Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita.Hiyo ni kutokana na kuthamini nafasi ya waamuzi wasaidizi,"amesema Ndimbo

Kwa mazingira hayo tuzo zitakazotolewa siku hiyo ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ni Bingwa,Mshindi wa Pili,Mshindi wa Tatu,Mshindi wa Nne, Mfungaji Bora,Timu yenye nidhamu,U20 Player (Tuzo ya Ismail Khalfan),Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Bora Msaidizi,Mwamuzi BoraKipa Bora,Kocha Bora,Goli Bora VPL,Best Eleven,pamoja na Mchezaji wa heshima.

Ndimbo amesema zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.

"Kila mwezi Kamati ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya vizuri kwa mwezi husika kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti kutoka kwa makocha waliopo katika viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.

"Wachezaji  ambao  walishinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu ni nimshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba). 

"Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari), mshambuliaji wa  Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa Majimaji, Marcel Kaheza (Aprili),"amesema Ndimbo.

Ambapo wachezaji hao kila mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king'amuzi cha Azam na fedha Sh.milioni moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.

RAIS WA SOKA WA GHANA KUKAMATWA

Akufo amefikia maamuzi ya kutoa agizo hilo kufuatia makala ya uchunguzi iliyofanywa ikimuhusisha Kwesi Nyantekyi kudaiwa kuhusika katika vitendo vya ulaghai.
Maamuzi hayo ya Akufo Addo kutangaza kukamakwa kwa Kwesi Nyantekyiyamewashitua wengi kutokana na mahusiano ya wawili hao ambapo kwa mujibu wa CITI FM ya Ghana inaeleza kuwa wana urafiki.

Simba, Yanga zatangaziwa dau la Salamba


By CHATIRY JAMES 
UONGOZI wa Lipuli FC, umesema unahitaji Sh50 milioni ili kumuachia mshambuliaji wao, Adam Salamba ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na timu mbalimbali za Ligi Kuu Bara. Timu za Simba, Yanga na Azam FC tayari zimeonyesha nia ya kumsajili Salamba, ambaye amefunga mabao manane Ligi Kuu Bara msimu huu. Mwenyekiti wa Lipuli, Ramadhan Mahano alisema wameshaanza mazungumzo na klabu za Azam na Simba ambazo zimeonyesha nia ya kumhitaji mchezaji huyo wa zamani wa Stand United. 
"Simba na Azam ndio timu ambazo zimeleta maombi mezani kwa ajili ya kumsaini Salamba tofauti na magazeti mengi yanavyoripoti kuwa tumeingia katika mazungumzo na Yanga, sio kweli Yanga tangu tumewakatalia hawajaonyesha nia," alisema.
 "Tunafanya mazungumzo na Simba na Azam na kila timu inafahamu ni dau gani tunalihitaji ili tuweze kuwaachia mchezaji wetu jambo, ambalo tunaamini ni la busara zaidi kwa sababu Salamba bado ana mkataba," alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Credit Mwanaspoti/Gazeti

MWIGULU NCHEMBA AMEFANYA ZIARA KISIWANI UNGUJA HII LEO

 Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh:Mwigulu Nchemba akikagua gwaride la askari mara baada ya kuwasili makao makuu ya jeshi la polisi zanzibar.
 Mapokezi yakiendelea kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi mara baada ya kuwasili kisiwani Unguja hii leo.
 Mwigulu Nchemba akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa jeshi la polisi hii leo zanzibar.
 Mwigulu akisalimiana na baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi waliopo visiwani Zanzibar.
 Waziri wa mambo ya ndani ya nchi akiongoza kikao cha ndani kilichohusisha viongozi wa juu wa jeshi la polisi Zanzibar.
 Mh:Mwigulu Nchemba akikagua moja ya majengo chakavu yanayohitaji ukarabati ndani ya eneo la Makao makuu ya jeshi la polisi Unguja.
 Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi akiwasili ofisi za Uhamiaji-Zanzibar hii leo.
 Mmoja wa maofisa wa idara ya Uhamiaji akitoa maelezo kwa Waziri Mwigulu Nchemba namna mchakato wa utoaji wa Vitabu vya kusafiria "Passport" vinavyotelewa katika ofisi hiyo.

 Waziri wa mambo ya ndani akiongoza kikao cha watendaji wa idara ya Uhamiaji visiwani Zanzibar hii leo,
 Waziri wa mambo ya ndani katika picha ya pamoja na maafisa wa juu wa idara ya Uhamiaji-Zanzibar.
 Mh:Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na watumishiwa idara ya Vitambulisho vya Taifa-NIDA -Zanzibar.
 Mwigulu Nchemba akizungumza na watumishi wa jeshi la polisi,NIDA na Uhamiaji katika Bwalo la polisi-Ziwani hii leo.
Katika mengi aliyozungumza nao,Mh:Mwigulu amesisitiza kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya madawa ya kulevya hasa katika usafirishaji majini na maeneo wanayouzia madawa hayo.
 Pia,Mwigulu Nchemba ameweka bayana kuwa ni lazima jeshi la polisi lifanye kazi kwa umoja wa hali ya juu ilikuhakikisha ulinzi na usalama unaendelea kuimarisha nyakati zote.
 Katika hatua nyingine,Waziri wa mambo ya ndani ametoa fursa kwa watumishi wa wa wizara anayoiongoza kutoa kero,changamoto au maoni ambayo yangetumika kuboresha utendaji wa idara anazoiongeza.Katika kero kubwa ambazo askari wameendelea kusisitiza ni makazi na maslahi na malimbikizo ya madeni ya uhamisho na upandshaji wa vyeo kwa wakati.
 Mmoja wa afisa wa idara ya mambo ya ndani akichangia maoni yake na kero zinazopaswa kurekebishwa ilikupambana na wahamiaji haramu katika mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mh:Turky ambaye ni Mbunge wa moja ya jimbo kisiwani Unguja akitoa neno la shukrani kwa waziri kwa namna alivyojitoa kuhakikisha anatatua kero za askari na watumishi wote wa wizara ya mambo ya ndani.
Mwisho,Waziri wa mambo ya ndani amekutana na askari wa jeshi la polisi waliostaafu kwaajili ya kusikiliza ushauri wao katika kuimarisha utendaji kazi wa idara za mambo ya ndani.
Pciha/Maelezo na Festo Sanga Jr.

MWIGULU NCHEMBA AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR MH:ALI MOHAMED SHEIN HII LEO

Mh:Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkaribisha Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mh:Mwigulu Lameck Nchemba hii leo Ikulu-Zanzibar alipomtembelea kwaajili ya mazungumzo.
 Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi.Mh:Mwigulu Nchemba akifanya mazungumzo na Mh:Rais wa Zanzibar kabla ya kuanza ziara ya kikazi visiwani humo iliyolenga kukutana na vikosi vya jeshi la polisi,NIDA,Uhamiaji n.k.
Wakiagana mara baada ya Mazungumzo.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.

KUTOKA MUHIMBILI

MWIGULU NCHEMBA AONYA WAKIMBIZI WANAOJIHUSISHA NA UBAGUZI ,UHALIFU NA WIZI

Waziri wa Mambo ya ndani akisikiliza ripoti ya Mkoa wa Katavi kutoka kwa kaimu Mkuu wa Mkoa huyo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Mpanda.Askari wa Jeshi la polisi kwa idara zote wakiimba wimbo wa maadili tayari kwa kumsikiliza Mh:Mwigulu Nchemba wilaya ya Mpanda Mjini.Waziri wa mambo ya ndani akiangalia tofali