A

A

Simba, Yanga zatangaziwa dau la Salamba


By CHATIRY JAMES 
UONGOZI wa Lipuli FC, umesema unahitaji Sh50 milioni ili kumuachia mshambuliaji wao, Adam Salamba ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na timu mbalimbali za Ligi Kuu Bara. Timu za Simba, Yanga na Azam FC tayari zimeonyesha nia ya kumsajili Salamba, ambaye amefunga mabao manane Ligi Kuu Bara msimu huu. Mwenyekiti wa Lipuli, Ramadhan Mahano alisema wameshaanza mazungumzo na klabu za Azam na Simba ambazo zimeonyesha nia ya kumhitaji mchezaji huyo wa zamani wa Stand United. 
"Simba na Azam ndio timu ambazo zimeleta maombi mezani kwa ajili ya kumsaini Salamba tofauti na magazeti mengi yanavyoripoti kuwa tumeingia katika mazungumzo na Yanga, sio kweli Yanga tangu tumewakatalia hawajaonyesha nia," alisema.
 "Tunafanya mazungumzo na Simba na Azam na kila timu inafahamu ni dau gani tunalihitaji ili tuweze kuwaachia mchezaji wetu jambo, ambalo tunaamini ni la busara zaidi kwa sababu Salamba bado ana mkataba," alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Credit Mwanaspoti/Gazeti

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako