A
MWANDISHI ATEKWA ARUSHWA, WAHUSIKA WADAKWA
Leo May 23, 2018 Ofisa itifaki katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Swalehe Mwindadi pamoja Mtunza kumbukumbu Amina Mshana wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha kwa kesi inayowakabili ya kumteka Mwandishi wa habari Lucas Myovela.
Awali watuhumiwa hao walikamatwa kwa tuhuma za Kumteka na kumshambulia mwandishi wa habari usiku wa kuamkia May 14, 2018.
KOCHA MSAIDIZI AKABIDHIWA SIMBA
atakayeiongoza timu hiyo kwenye michuano ya SportPesa, inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini Kenya. Taarifa kutoka Simba zinadai kuwa, wataachana na Kocha wao Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre, baada ya Ligi ya msimu huu kumalizika Jumatatu ya wiki inayokuja. Taarifa hizo zinadai kuwa, uongozi umeona mshahara wa Mfaransa huyo ni mkubwa sana ikilinganishwa na uwezo wake, hivyo wanafikiria kuachana naye.
Mfaransa huyo, ambaye alisaini mkataba wa miezi sita inayomalizika mwezi ujao, huenda akatimkia Cameroon, ambako ameomba kibarua cha kuinoa timu ya Taifa ya nchini humo, kama Simba wataamua kuachana naye. Kigogo mmoja ndani ya timu hiyo ameliambia DIMBA Jumatano kuwa, kwa sasa akili zao ni kutafuta mbadala wa Mfaransa huyo, ili asaidiane na Djuma. “Ni kweli kuna uwezekano mkubwa tukashindwa kuendelea na Pierre (Lechantre), kwani mshahara wake ni mkubwa sana, tunachofikiria ni kutafuta kocha mwingine mkuu, lakini mwenye uwezo mkubwa. “Baada ya kumalizika kwa Ligi, timu itakuwa na maandalizi ya kwenda Kenya kushiriki michuano ya SportPesa na kocha wetu msaidizi Masoud Djuma ndiye atakayebeba jukumu hilo,รข€� alisema.
DIMBA Jumatano lilimtafuta Mfaransa huyo ili kuzungumzia hatima yake, hakuwa na mengi zaidi ya kusema yeye kwa sasa hawezi kusema lolote, kwani mambo yake yanasimamiwa na mawakala wake. “Kwa sasa siwezi kusema mengi, kwani ninao mawakala wangu wanaoshughulikia mambo yangu, nadhani kila kitu kitakuwa wazi,” alisema.
Nani kukatwa nani kubaki???Mbowe Kufanya Mabadiliko ya Baraza Lake Mawaziri.
Na Mwandishi,
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe anatarajiwa kufanya mabadiliko ya baraza lake kivuli la mawaziri.
Katika mabadiliko hayo, Mbowe anatarajiwa kuingiza sura mpya, kuhamisha baadhi wizara, wengine kubaki kwenye nafasi zao huku akiwatoa baadhi yao.
Kwa mujibu vyanzo mbalimbali ndani ya kambi hiyo, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anatarajiwa kulitangaza baraza hilo wakati wowote.
Baraza kivuli alilolitangaza Februari 5, 2016 bungeni jijini Dodoma lilikuwa na wizara 18 likijumuisha vyama washirika wa Ukawa vyenye wabunge; NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF.
CUF kwa sasa imegawanyika katika pande mbili; upande unaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na upande wa katibu mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuzingatia ongezeko la
Kesi Ya Babu Tale Yaahirishwa, Arudishwa Mahabusu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale maarufu Babu Tale, leo Mei 23, 2018 saa 6 mchana amefikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi inayomkabili, akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Babu Tale, ambaye pia ni meneja wa mwanamuziki maarufu wa
WACHEZAJI 30 KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA
Na Agnes Francis Blogu ya Jamii.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)limetangaza majina ya wachezaji 30 katika kuelekea mwisho wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ambao watawania Tuzo za Mchezaji Bora mwaka huu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa TFF Clifford Ndimbo amesema utaratibu huo hufanyika kila mwaka baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Vodacom.
Ndimbo amefafanua wachezaji hao 30 watachujwa na kubaki 10 na baadae watabaki wachezaji wa tatu wataoinga hatua ya fainali ili kumpata Mchezaji bora kwa msimu huu.
Amewataja wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Habibu Kyombo (Mbao),Khamis Mcha,(RuvuShooting),Yahya Zayd(Azam),Razack Abalora(Azam), Bruce Kangwa(Azam) Aggrey Morris(Azam),Himid Mao (Azam),Awesu Awesu(Mwadui) na Adam Salamba(Lipuli).
Wengine ni Mohammed Rashid(Prisons), Shafiq Batambuze(Singida),Mudathir Yahya (Singida), Marcel Kaheza(Majimaji),Ditram Nchimbi(Njombe Mji) na Eliud Ambokile(Mbeya City).
Pia Shaaban Nditi(Mtibwa), Tafadzwa Kutinyu(Singida) Ibrahim Ajibu(Yanga), Gadiel Michael(Yanga),Papy Tshishimbi(Yanga),Kelvin Yondani(Yanga),Obrey Chirwa(Yanga),Aishi Manula(Simba), Emmanuel Okwi(Simba),John Bocco(Simba), Jonas Mkude(Simba),
Erasto Nyoni(Simba),Shiza Kichuya(Simba),Asante Kwasi(Simba),Hassan Dilunga(Mtibwa).
"Mchakato wa kupata mchezaji bora unatarajia kufanyika Juni 23 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ambapo msimu huu kutakuwa na washirika wengine Azam Tv, Benki ya KCB na Premier Bet,"amefafanua
Pia amesema licha ya tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, kutatolewa tuzo mbalimbali, ambapo kwa mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine imeongezwa ikiwa ni katika uboreshaji
"Tuzo iliyoondolewa ni ya Mchezaji Bora wa Kigeni na imefanyika hivyo ili kuwapa fursa wachezaji wote kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL badala ya kuwatenganisha, vile vilee msimu huu imeongezwa Tuzo ya Mwamuzi Bora Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita.Hiyo ni kutokana na kuthamini nafasi ya waamuzi wasaidizi,"amesema Ndimbo
Kwa mazingira hayo tuzo zitakazotolewa siku hiyo ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ni Bingwa,Mshindi wa Pili,Mshindi wa Tatu,Mshindi wa Nne, Mfungaji Bora,Timu yenye nidhamu,U20 Player (Tuzo ya Ismail Khalfan),Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Bora Msaidizi,Mwamuzi BoraKipa Bora,Kocha Bora,Goli Bora VPL,Best Eleven,pamoja na Mchezaji wa heshima.
Ndimbo amesema zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.
"Kila mwezi Kamati ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya vizuri kwa mwezi husika kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti kutoka kwa makocha waliopo katika viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.
"Wachezaji ambao walishinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu ni nimshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).
"Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari), mshambuliaji wa Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa Majimaji, Marcel Kaheza (Aprili),"amesema Ndimbo.
Ambapo wachezaji hao kila mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king'amuzi cha Azam na fedha Sh.milioni moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.
Subscribe to:
Posts (Atom)