A

A

Tuesday, February 9, 2016

MVOMERO KWA VAMIWANA FIELD MARSHALL,MBUZI 77 WAKATWAKATWA MAPANGA,MWIGULU AANZA SAFARI YA KUTATUA MGOGORO

Mh:Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi  Ndg,Mwigulu Lameck Nchemba akiwasili kata ya Hembeti,Kijiji cha Dihinda mapema hii leo kuangalia madhara na kuchukua hatua dhidi ya uhusiano mbaya uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopelekea kuuawa kwa mbuzi Zaidi ya 70 kwa kukatwakatwa mapanga wilayani Mvomero.Mh;Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Hembeti wilaya ya Mvomero wakati wa hatua za awali za kutafuta suluhu ya kuondokana na mapigano ya wakulima nawafugaji yaliyosababisha Mbuzi zaidi ya 70 kukatwa katwa usiku wa kuamkia tar 9/02/2016 katika kitongoji cha Dihinda.
Katika Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016 kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.
Wakati huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.Mh:Mwigulu Nchemba akipokea baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro kuhusiana na tukio la mapigano ya wakulima na wafugaji eneo la Mvomero.Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga.Mwigulu Nchemba akishuhudia madhara yaliyotokana na ugomvi wa wakulima na wafugaji kitongoji cha Dihinda uliopelekea mbuzi hawa kukatwakatwa.Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na mama mjane aliyejeruhiwa na mbuzi wake kukatwa katwa mapanga  na watu wanaodhaniwa ni wakulima katika kitongoji cha Dihinda.Sehemu ya Mbuzi waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima wilayani Mvomero.Mwigulu akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakiangalia madhara yaliyosababishwa na uhusiano mbaya kati ya wakulima na wafugaji eneo la kata ya Hembeti.Waziri wa Kilimo.Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakichanja mbuga za kijiji cha kigurukirwa wakati wa kukagua madhara yaliyotokana na uhusiano mbaya kati ya wakulima nawafugaji wilayani mvomero hii leo.
Picha na Sanga Festo Jr.
 

Monday, January 4, 2016

NEWS ALERT:MWIGULU NCHEMBA ATIMUA VIGOGO WALIO RAMBA BILION 5.7 ZA UJENZI WA MACHINJIO RUVU

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa Ujenzi wa machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu mapema hii leo.Sehemu ya jingo lililobaki kama Gofu mara baada ya kutelekezwa na Uongozi wa Bodi ya ranchi za Taifa(NARCO)Mwigulu Nchemba akishangaa namna mali hii ya Umma ilivyotekelezwa.Mwigulu akiwa na jopo la wataalam wakiendelea kutathimini hasara iliyojitokeza kutokana na ujenzi mbovu wa machinjio ya kisasa hapa Ruvu.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Chalinze Mh.Ridhiwani wakisikiliza kwa makini sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa.Anayetoa maelezo wa mwisho kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd.Bwire.
Sehemu ya jingo ikiwa imetelekezwa bila kuendelezwa kiujenzi.Hii ni sehemu ya ukuta wa jingo hilo ambao umekatika kutokana na kukaa muda mrefu bila kuendelezwa.Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu.Mh.Ridhiwani kikwete Mbunge wa Chalinze akitoa malalamiko yake kwa Waziri.Mwigulu Nchemba kuhusu kukosekana kwa mahusiano mazuri kati ya wamiliki wa ranchi na wananchi wanaozunguka ranchi ya Ruvu.Kwa mbali hili ndio jengo la machinjio ya kisasa lililokuwa linajengwa na hatimaye kutelekezwa bila kuendelezwa tangu mwaka 2010.Mh:Mwigulu Nchemba akiteta jambo na viongozi wanaohusika na kulinda baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa kwaajili ya ranchi hiyo ya kisasa.Mh;Mwigulu Nchemba akioneshwa baadhi ya Ng'ombe wanaopatikana kwenye ranchi hiyo.Mwigulu Nchemba akiwa kazini kwenye shamba la Mifugo la Ruvu hii leo.Mwigulu Nchemba akidadisi utunzaji wa maji ya Mifugo inayopatikana ndani ya ranchi ya Ruvu.
 
Wakati Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya Rais.J.P.Magufuli kwa speed yake ya uchapa kazi,Mawaziri wake pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za maendeleo ya Nchi yetu.
Hii leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.
Katika hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu Nchemba amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo,Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.
Waziri huyo wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila kuendelezwa,Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO(kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu Nchemba ambaye baada ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo aliamua ifuatavyo.
Kwanza,Mwigulu Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo la ranchi ya ruvu.
Pili,Mwigulu Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake.
Pia,waziri huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
Mwisho,Nchemba amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7 wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.
Sambamba na hatua hizo,Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya nchi yetu,Mbali na hapo,serikali ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.
Picha/maelezo na Festo Sanga Jr

Saturday, January 2, 2016

TIMUA TIMUA MACHINJIO YA VINGUNGUTI NA MNADA WA PUGU,MWIGULU ATIMUA MKUU WA MNADA NA WATUMISHI KADHAA WALIOHUSIKA KUIBA KODI YA SERIKALI

FMh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mh:Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo.Mwigulu Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh:Simbachawene wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mh:Simbachawene wakielekea kuzungumza na wananchi wanaotumia Machinjio ya vingunguti.Mawaziri kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana jambo.Mkutano ukiendelea wa kutoa majawabu kuhusu changamoto za Machinjio ya Vingunguti.Mh:Simbachawene akiwaagiza watumishi wote wa Machinjio ya Vingunguti kuripoti ofisini kwake Jumanne wakiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.Furaha ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za awali,wananchi wanasukuma gari la Mh:Mwigulu Nchemba kama ishara ya kukubali hatua alizochukua.
 
Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa Mh:Rais J.Magufuli mara baada ya tukio la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja mifugo.
Awali,Mh.Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye mifugo,lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo.
Hii leo mapema majira ya saa 3:asubuhi,Mwigulu Nchemba anarejea tena kwenye machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili ambao ni Mh:Simbachawene(TAMISEMI) na Mh:Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo.
Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.
Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tar 24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia sasa,Vilevile wahakikishe jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Pili,Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa pugu,badala ya hapo makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.
Tatu,Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi(wadau) kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa kwaajili ya kutunzia nyama,Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa.
Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.
Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mh:Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na mkurugenzi kwaajili ya hatua Zaidi.
Simbachawene ameenda mbali Zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana na wingi wa watu wanaotumia machinjio hayo.
Kwa upande wa Afya,Naibu waziri wa Afya Mh.Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg.Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo,Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na Uongozi wa machinjio utenge ofisi maalu ya kupima watu hao.
 
Picha/Maelezo na Festo Sanga

ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE,MWIGULU NCHEMBA ATUA MACHINJIO YA VINGUNGUTI USIKU HUU..AKUTANA NA UCHAFU WA KUTISHA

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba akisikiliza kero za wadau wa machinjio ya Vingunguti usiku huu wa January 1/01/2016.Mwigulu Nchemba akishuhudia Ng'ombe aliyetayari kwa taratibu za kuchinjwa kwaajili ya kitoweo.
Mbuzi wakiwa tayari kwaajili ya kuchinjwa kwenye machinjio hayo ya Vingunguti.Mbuzi hawa asilimia kubwa wanatoka mnada wa pugu ambao Ushuru wake unakusanywa na serikali kuu.Waziri Mwigulu Nchemba akikagua maeneo ya machinjio hayo usiku huu.
Mwigulu Nchemba akitoa maagizo kwa uongozi wa Machinjio ya Vingunguti kukutana kesho saa 2:00 asubuhi kwa wahusika wote wenye dhamana na Machinjio hayo,Mkutano utafanyika eneo la Machinjio hayo.
 
Katika hatua ya kushitukiza,Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amefanya ukaguzi wa Machinjio ya Vingunguti usiku huu.
Mh.Mwigulu Nchemba amefika kwenye Machinjio hayo usiku huu ilikushuhudia Mifugo ikiandaliwa kwaajili ya kitoweo cha wananchi.Uchinjaji wa Ng'ombe na Mbuzi katika machinjio haya hufanyika nyakati za Usiku kuanzia saa 4 hadi 10 alfajiri.
Mbali na kusikiliza kero na maoni ya wananchi kuhusu uendeshwaji wa Machinjio hayo,Mwigulu Nchemba ameshuhudia utafunwaji wa kodi ya serikali inayokusanywa kwenye mnada wa pugu.
Utafunwaji huo unatokana na uandikaji wa kibali cha mifugo michache kuja Machinjioni ili hali mifugo Zaidi huingizwa machinjioni bila kibali.Matharani hii leo Mh.Waziri ameshuhudia Ng'ombe waliotoka mnada wa pugu ambao wameshalipiwa kodi wakiwa 1450 lakini kibali chake kimeandikwa Ng'ombe 300 tu.Inamana kuna ng'ombe 1150 wamelipiwa ushuru lakini machinjioni kimeletwa kibali cha ng'ombe 300 wakati kwa kuwahesabu ng'ombe hao wanazidi 1000.
Kutokana na hali hiyo,Mh.Waziri ameagiza wahusika wote kufika kesho kwenye mkutano wa asubuhi kwaajili ya hatua stahiki kuchukuliwa,Mwigulu amesisitiza kuwa kwa mtu yeyote mwenye dhamana na kusimamia sekta ya kilimo,Mifugo na Uvuvi afanya kwa mujibu wa sharia,vinginevyo hakutakuwa na huruma kwa wanaohujumu.
 

Wednesday, December 23, 2015

MWIGULU NCHEMBA AWATAFUTIA MALISHO WAFUGAJI MKOA WA KAGERA,WIZARA YA MALI ASILI YAAHIDI KUACHIA MAPORI KADHAA

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiwasili eneo la mkutano uwanja wa Mnadani wilayani Ngara kuzungumza naWafugaji/wakulima mapema hii leo.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mali asili Mh.Ramo Makani ambaye waliongozana naye kwenye mkutano huo kama wadau wa wafugaji kwenye mapori yanayosimamiwa na Mali Asili.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wafugaji/Wakulima waliokusanyika kutoka wilaya ya Ngara,Muleba,Karagwe n.k
 
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akimuomba maeneo ya Malisho ya wafugaji yaongezwe kutoka mapori ya akiba ambayo kwa sasa yanawezwa kutumiwa na wafugaji wa mkoa wa kagera.
Mh.Ramo Makani akimhakikishia Mh.Mwigulu Nchemba kuwa Wizara ya Mali Asili itafanya kazi bega kwa bega na Wafugaji na wakulima hususani kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi za Mali asili na wanyama.
 
Mapema leo Desemba 22/2015, Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amekutana na Wananchi wafugaji na wakulima wa wilaya za Ngara,Karagwe,Biharamulo,Kyerwa n.k Mkoani Kagera kuzungumza nao adhima yake ya kutatua tatizo la malisho kwa wafugaji wanaozunguka mapori tengevu yanayopatikana Mkoa wa Kagera.
Katika mkutano uliofanyika Uwanja wa Mnadani (Benaco) Ngara,Mwigulu Nchemba amesikiliza changamoto zinazowakabili wafugaji kupitia Chama cha Wafugaji wa kanda ya Ziwa (CHAWAKAZI) kilichosajiliwa mwaka 2002 kinachojumuisha wafugaji kutoka Kahama,Bukombe,Geita,Chato,Ngara,Muleba n.k.,Changamoto kubwa ambayo wafugaji wameiwasilisha kwa Mh.Waziri ni uonevu na unyanyasaji unaofanywa na askari wa wanyamapori wanaolinda Mapori ya akiba ya Burigi,Kimisi,Rumanyika,Muyowosi na Kigosi.Askari wanyamapori wanashutumiwa kujihusisha na utesaji wa ng'ombe wanaokamatwa maeneo karibu na mapori hayo,Ulipishwaji wa faini zisizohalali kwa madai ya ng'ombe kuingia kwenye hayo mapori.
Zaidi,Wafugaji wameomba serikali iwapatie maeno ya mapori ambayo kwa sasa yanaweza kuwa sehemu ya lanchi ndogo za wafugaji.Pia wameoimba serikali iachane na operation ya kuwaondoa wafugaji kutoka kwenye maeneo yanayotumika kuchunga ng'ombe katika pori la Burigi.
Akitoa majawabu ya changamoto hizo,Mwigulu Nchemba amewasisitiza wananchi mambo makuu mawili(2).Kwanza watambua kuwa serikali imedhamiria kutatua migogoro yote inayoikabili sekta ya ufugaji,kilimo na uvuvi,Hili linakwenda sambamba na agizo la Mh.Rais  J.Magufuli kuwa wakulima na wafugaji wapatie suluhisho la kudumu,Pili amewaomba wafugaji na wakulima kuheshimu hifadhi zilizotengwa ilivizazi vijavyo viwezekunufaika nazo.Kwa upande wa maeneo ya malisho,Mwigulu Nchemba amemuomba Naibu Waziri wa Mali Asili kupitia ofisi yake iangalie uwezekano wa kuyapitia upya mapori tengevu ili baadhi wapewe wafugaji na wakulima kwa shughuli zao.
 
Akioneshwa kuguswa na changamoto za wafugaji wa mkoa wa Kagera na Tanzania yote,Naibu waiziri wa Mali Asili ametangaza kusitishwa kwa operation za kuwaondoa wafugaji kwenye maeneo wanayochungia mifugo yao,Pilia ameahidi kupitia ofisi yake itafanya haraka iwezekanavyo utaratibu unaoendelea wa kupitia mapori 17 ilikutoa maeneo kwa watu waweze kufanya shughuli zao(Kilimo,Mifugo n.k)
Mh.Ramo kupitia hadhara hiyo amelaani kitendo kilichofanywa na watu wanaodaiwa kuwa ni kutoka Mali Asili waliofyeka ekari 150 za mahindi wilaya ya Mbozi."Ni jambo lisilokubalika kabisa,na kupitia mkutano huu naagiza kama kuna wakulima wamelima eneo ambalo linadhaliwa ni hifadhi waachwe hivyohivyo hadi hapo mazao yatakapo komaa na utaratibu mwigine utakapotolewa"
Lakini pia,Mh.Ramo amewaomba askari wanyamapori kuzingatia maadili ya kazi yao,kwa wale baadhi wanaojihusisha na utesaji,Unyanyasaji na kujipatia fedha haramu kwa kukamata mifugo au wakulima waache mara moja,Serikali inakwenda kuchukua hatua kuhakikisha askari wote wanafanya kazi kwa kuheshimu sharia za nchi.
Imeandikwa/Picha na Festo Sanga (R)

Wednesday, December 16, 2015

MWIGULU NCHEMBA "NAHITAJI MAJAWABU SIO MAJIBU"

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akisalimiana na watumishi wa wizara yake mapema hii leo alipowasili ofisini kwaajili ya kuzungumza na watumishi wa wizara hiyo.Mh.Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa zira ya Kilimo,Uvuvi na Mifugo hii leo.Waziri na Naibu waziri Mh.Ole Nasha wa Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi wakisaini vitabu vya wageni wakati wa kufahamiana na watumishi wa wizara hiyo hii leo.Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Lameck Nchemba Madelu akizungumza na Watumishi wa wizara yake hii leo,Mwigulu amewaagiza na kuwasisitiza watumishi wote wa wizara yake waliopo Makao makuu na mikoani kuwa "Ninahitaji tufanye kazi kwa kiwango cha juu,Wote tunazijua changamoto za wakulima,Wafugaji na wavuvi,sitegemei kusikia pembejeo hazifiki kwa wakati,Kwa wakati huu nahitaji kuona MAJAWABU sio MAJIBU"
Imeandikwa/Picha na
Festo Richard Sanga