A

A

Ujumbe kutoka FRELIMO Ulipotembelea Ofisi za CCM Lumumba

Kushoto ni Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania,Katikati Mh:Mwigulu Nchemba Naibu katibu Mkuu CCM Bara na Kulia ni Bi,Nyeleti Mondlane ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha FRELIMO Nchini Msumbiji.Ujumbe huu kutoka Msumbiji ulitembea Ofisi za CCM lumbumba jana Tar.18/09/2014 CCM na FRELIMO ni Vyama rafiki na vyote vimeshiriki katika harakati za Ukombozi.Hivi sasa Nchini Msumbiji wapo kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa RAIS,ambapo FRELIMO imemsimamisha Filipe Nyussi kuwa Mgombe URAIS.Kihistoria Nyussi amepata kusoma Kusini mwa Tanzania mji wa Tunduru na amepata mafunzo ya kijeshi Kambi ya Nachingwea.Naibu Katibu Mkuu CCM Bara akimvalisha skafu ya Tanzania Bi. Nyeleti Mondlane kutoka MSumbiji chama cha FRELIMONaibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh,Mwigulu nchemba akiwa katika picha ya Pamoja na Ujumbe kutoka Msumbiji-FRELIMO uliofika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi Lumumba Dsm kwaajili ya kuzingumza mambo mbalimbali ikiwamo Uchaguzi wa Msumbiji unaotegemewa kufanyika mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako