Waliosababishia Serikali hasara ya bn 40/- kukiona
Naibu Waziri wa Fedha, Mungulu Nchemba
Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mungulu Nchemba,
akisema wakuu hao pamoja na waajiri wametumia mwanya wa wafanyakazi wao
katika ubadhirifu wa fedha kwa maslahi yao binafsi.
Kadhalika, wizara inawataka maafisa utumishi na waajiri kuhakiki
upya taarifa wanazoweka katika mfumo ni sahihi ili watumishi wao
wawekewe malipo yao katika akaunti kwa wakati mwafaka.
“Zoezi hili ni endelevu, hivyo tumebaini tatizo na tunatafuta njia
ya kulimaliza na hii tuliyowaagiza waajiri itakuwa njia ya kutokea,
hivyo tutalinganisha taarifa zao na muda wa watumishi wao tuone tatizo
lilikuwa wapi,” alisema.
Pia, alisema hakuna sababu ya wizara kuendelea kulipa malipo hewa
wakati kuna kundi la wafanyakazi katika taasisi na mashirika hayo, ambao
kazi yao ni kuhakiki mafaili na wanalipwa mishahara mikubwa huku wale
wanaojituma wakiendelea kujaziwa mishahara hewa.
Aliwaagiza waajiri na maafisa hao kufikisha orodha ya majina ya
watumishi wakiambatanisha na taarifa sahihi ya mishahara tarehe za
mwanzo za kila mwezi zifanyiwe kazi mapema ili kuwepo na uwajibikaji
katika sehemu za kazi.
Alisema fedha za miradi katika taasisi hizo zitatolewa kulingana na
mchanganuo wa malipo yao, “Hatuwezi kuendelea kutoa malipo hewa
kinyemela tena, hivyo wataalamu wetu watashirikiana na wakuu hao wa
maradi kuangalia kama unakidhi kutekelezewa,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako