A

A

MGOMBEA WA URAIS WA MSUMBIJI KWA TIKETI YA FRELIMO AWASILI NCHINI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege ,jijini Dar es salaam.
  Katibu NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na  Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege ,jijini Dar es salaam.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusiakiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo atakuwa na ziara ya siku 4 nchini Tanzania.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusia akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana nyumbani kwa Mwalimu Nyerere ,Msasani Dar es Salaam.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani,jijini Dar es salaam.
 Mama Maria Nyerere akisalimiana na Samora Machel Jr nyumbani kwa Mama Maria Nyerere,Msasani Dar es Salaam.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akiondoka nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam baada ya kupita kumsalimia mara baada ya kuwasili nchini.(Picha na Adam Mzee).

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako