WAZIRI
Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ameutaka uongozi
mpya wa Klabu ya Simba kutolipiza kisasi au kufukua maovu ya uongozi
uliopita na badala yake kujikita katika kuweka mikakati ya kuendeleza
klabu.
Lowassa
alisema hayo ofisini kwake Dar es Salaam jana alipotembelewa na Rais
mpya wa Simba, Evans Aveva. Lowassa amemtaka Aveva kuunganisha wanachama
wa Simba kwa manufaa ya soka la Tanzania
Aidha,
aliwataka viongozi wa klabu kubwa nchini kusajili zaidi wachezaji wa
nyumbani na kuachana na tabia ya kukimbilia kusajili wachezaji wa kigeni
kwani hiyo inadhoofisha uimara wa timu ya taifa.
Lowassa
alitolea mfano timu ya Taifa ya England ilivyofanya vibaya katika
fainali za Kombe la Dunia la Fifa akisema inatokana na klabu za Ligi Kuu
ya nchi hiyo kuwa na wachezaji wengi wa kigeni kuliko wa ndani.
Kwa
upande wake, Rais huyo wa Simba, Aveva alisema uongozi wake umejipanga
kuwekeza katika vijana ili kupunguza gharama za kusajili wachezaji wapya
kila msimu.
Pia
alimweleza Lowassa kuwa wanatarajia kufungua hosteli katika kipindi
kifupi kijacho katika eneo jipya la klabu hiyo Bunju katika Manispaa ya
Kinondoni.
Amesema
awamu ya pili ndiyo itakuwa ya ujenzi wa uwanja ambapo alimwomba Lowassa
kukubali mwaliko wa kufanya harambee ya kukusanya fedha za ujenzi wa
uwanja huo wakati ukifika.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako