A

A

SHUKRANI


SHUKRANI
Tarehe 1 Juni 2014 tuliondokewa na Mama yetu mpenzi Bi. Shida Salum. Mauti yalimkuta mama katika Hospitali ya AMI, Masaki jijini Dar es Salaam na mazishi kufanyika mjini Kigoma mnamo tarehe 2 Juni 2014.
Tunapenda kutoa shukrani zetu za
dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshiriki nasi katika msiba huu mkubwa kwetu. Tunawapa shukrani zetu madaktari na wahudumu wa Hospitali za Apollo (Cancer and Main) jijini Chennai nchini India na AMI jijini Dar es Salaam kwa juhudi zao kubwa za kumhudumia mama yetu. Tunatoa shukrani kwa Imam wa Msikiti wa Maamur Dar es Salaam na Sheikh wa Mkoa Kigoma Alhaj Hassan Kiburwa kwa ibada ya maiti.
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Uongozi mzima wa Bunge Maalum la Katiba, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mkoa wa Kigoma na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kwa ushirikiano mkubwa waliotupa katika mtihani mkubwa uliotufika. Tunashukuru wote waliofika Kigoma kwenye mazishi na wale waliotuletea salaam za rambirambi. Mwenyeji Mungu atawalipa kheri na kuwafanyia wepesi, Inshaallah.
Ibada ya 40 (Hitma) ya mama itafanyika nyumbani kwake Tabata Bima (Flats za NSSF) jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 12 Julai, 2014 kuanzia saa Kumi na Moja jioni (kabla na baada ya sala ya Magharibi).
INNA LILLAH WAINA ILAIH RAAJIUN

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako