Na MOblog Team
Polisi
Kanda Maalum Dar es Salaam inawashikilia watuhumiwa wawili wa ujambazi
wanaohusishwa na mauaji ya mtawa wa kaniasa Katoliki Sista Clezensia
Kapuli,
Zaidi ya watuhumiwa hao pia watu wengine sita wanashikiliwa wakihusishwa na matukio mbali mbali ya ujambazi nchini.
Hayo
yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar esSalaam
Kamishna Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari,aliwataja
majambazi wanaohusishwa na mauaji ya Sista Kapuli kuwa ni Manase
Ogenyeke “mjeshi” (35) mkazi wa Tabata Chang’ombe na Hamis Shaban
“Carlos” mkazi wa Magomeni mwembechai
Wengine
waliokamatwa kutokana na matukio ya ujambazi ni Beda Mallya miaka (37)
mkazi wa Mbezi msakuzi, Michael Mushi (50), Sadick Kisia (32), Elibariki
Makumba (30), Nurdini Suleiman (40) pamoja na Mrumi Salehe (38).
Majambazi
hao wamekamatwa kutokana na oparesheni kali inayoendelea jijini Dar es
Salaam baada ya kifo cha mtawa huyo aliyefariki dunia mnamo Juni 23
mwaka huu.
Kova
alisema majambazi hao wawili licha ya kuhusishwa na tukio la kifo cha
mtawa huyo, pia wanahusika na tukio la uporaji fedha katika benki ya
Barcrays tawi la Kinondoni.
“Majambazi
hawa walipora mamillioni ya fedha na huyu Ogenyeka ndiye aliyeendesha
pikipiki akimbeba jambazi mwenzake ambaye alikuwa na fuko hilo la fedha
na kutoroka nazo pia Shabani alikuwa ndiye kiongozi katika tukio hilo,”
alisema.
Aidha
alisema kuwa jeshi la Polisi bado linawatafuta watuhumiwa wengine
wawili katika tukio la mtawa na mmoja kwa jina maarufu Leonard Mollel
katika tukio la Barcrays.
Kova
alitoa wito kwa wananchi, wafanyabiashara kuachana na mazoea ya
kusafirisha fedha kienyeji badala yake watumie njia za kisasa zilizopo
sasa nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako