KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA RAHABU KIHANIKU (60) MKAZI WA KIJIJI
CHA KIKOTA AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA
SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI
YENYE NAMBA ZA USAJILI T.343 CMQ AINA YA HONDA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA
NDULA MWASANGAJA (32) MKAZI WA MTAA WA BAGAMOYO –TUKUYU.AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI
KATIKA KIJIJI CHA KIKOTA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU.AIDHA
KATIKA AJALI HIYO MTOTO ANGEL OSWARD (02) MKAZI WA KIKOTA ALIYEKUWA
AMEBEBWA NA MAREHEMU AMEVUNJIKA MGUU WA KUSHOTO NA AMELAZWA HOSPITALI YA
SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA
AMEKAMATWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA
PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA MAENEO YENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING]
ILI KUEPUKA AJALI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU
MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, MWENYE
UMRI KATI YA MIAKA 19-20 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
GARI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA 22:14 USIKU KATIKA
MTAA WA MBILINYI – SAE, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA
WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA GARI
MARA BAADA YA AJALI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE
NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE
MWENYEWE.
TAARIFA ZA MISAKO:
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA KWA KOSA LA KUPATIKANA
NA BHANGI. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1. JELY EVARIST (24) MKAZI WA
MWANJELWA 2. STAFORD NGENZI (21) MKAZI WA MWANJELWA, 3. ALAN AGUSTINO
(23) MKAZI WA ILEMI 4. ASIFIWE ABSOLOM (22) MKAZI WA JUA KALI 5. DATI
SAMWEL (24) MKAZI WA MWANJELWA 6. MWAKISYE NAZARETH (23) MKAZI WA
MWANJELWA NA 7. MICHAEL EZEKIEL (40) MKAZI WA NZOVWE.
WATUHUMIWA
HAO WALIKAMATWA KATIKA MAENEO TOFAUTI JIJINI MBEYA WAKIWA NA BHANGI
YENYE UZITO WA GRAM 429. MSAKO ULIFANYIKA KATIKA MAENEO YA JUA KALI,
MAKUNGULU NA MAJENGO MAPYA, KATA ZA ILEMI NA NZOVWE, TARAFA ZA SISIMBA
NA IYUNGA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA 23:30. WATUHUMIWA NI
WATUMIAJI NA WAUZAJI WA BHANGI.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA WATU AU
MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA
KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako