Na Francis Godwin Blog.
DIWANI
wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kata ya Lupingu wilaya
ya Ludewa mkoani Njombe John Kiowi amempongeza mbunge wa jimbo la
Ludewa Deo Filikunjombe kwa jitihada zake anazozifanya katika
kuwapelekea maendeleo wananchi wa Ludewa huku akiwashangaa wapinzani
wanaopinga jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali ya chama
cha Mapinduzi (CCM) na kudai kuwa yeye si mpinzani wa uchwara wa
kupinga maendeleo .
Akizungumza
na wanahabari jana wakati wa zoezi la mbunge Filikunjombe na
diwani huyo kushiriki na wananchi wa kata ya Lupingu kuchimba
mashimo ya nguzo za umeme na kusimika nguzo hizo za umeme , Kiowi
alisema kuwa ni zaidi ya wabunge watano wamepata kuliongoza
jimbo hilo la Ludewa ila ni mara yake ya kwanza kuona mbunge
akishiriki bega kwa bega na wananchi wake kuchimba mashimo kama
ambavyo mbunge huyo anafanya .
"
Jamani wananchi kwanza ni jambo la kumpongeza mbunge wetu mbali ya
kuhimiza wananchi ila mwenyewe pia amekuwa mstali wa mbele katika
kushiriki tofauti na wana siasa wengine ambao muda wote wao ni watu
wa majukwaani ila vitendo sifuri .....nasema Ludewa imempata mbunge
na niweke wazi hapa mimi sio mpinzani hivi tujiulize wenyewe
nikisema mimi ni mpinzani napinga nini hapa haya maendeleo ni kwa
faida yangu na wananchi wote sasa kama mbunge wa CCM wanafanya kuna
haja ya upinzani hapa "
Kiowi
alisema kuwa ataendelea kufanya kazi na mbunge Filikunjombe ikiwa ni
pamoja na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata yake kwani
chama chake cha TLP katika kata ya Lupingu kinatekeleza ilani ya
CCM ambacho ndicho chama kilichopo madarakani na peke yake bila
kumtegemea mbunge hawezi kufanya lolote.
Diwani
Kiowi ambae alikuwa amevalia sare za CCM katika shughuli hiyo ya
maendeleo alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa yeye si mpinzani ila
ni mpenda maendeleo hata sare za CCM zinazotolewa na mbunge
Filikunjombe amekuwa akizivaa na amekuwa mstali wa mbele kumpongeza
mbunge huyo kutokana na kuwa mbunge wa mfano kwa kufanya kazi bila na
makundi yote .
Hata
hivyo diwani huyo alisema kuwa katika suala la maendeleo hata kuwa
tayari kuona watu wachache wakimkwamisha mbunge huyo kwa kushindwa
kuunga mkono jitihada zake katika kuwaletea maendeleo na kudai kuwa
kwa upande wake anaona wapinzani ni wana CCM wenyewe wasiopenda
kujivunia maendeleo makubwa mbayo mbunge Filikunjombe ameyapeleka
Ludewa .
Kwa
upande wake mbunge Filikunjombe mbali ya kumpongeza diwani huyo wa
TLP kwa kushiriki vema katika shughuli za maendeleo bado alisema
kuwa ni wapinzani wachache nchini ambao wanajitoa kama diwani huyo
katika shughuli za maendeleo zinazoitishwa na mbunge wa CCM
Alisema
yapo baadhi ya maeneo wabunge ama madiwani wa upinzani wamekuwa ni
watu wa kupinga kila jambo linalofanywa na mbunge ama diwani wa CCM na
wengine wasiokuwa na uzalendo na Taifa wamefikia hatua ya kubeza
hata jitihada zinazofanywa na Rais Dr Jakaya Kikwete katika kuliletea
maendeleo Taifa jambo ambalo si la kizalendo hata kidogo na kuwa huo
si upinzani wa kweli.
"
Nataka kusema hivi wakati wa kampeni ndio wakati wa kupingana kisera
ila baada ya chaguzi hakuna haja ya kuendelea kupingana ni kuwa
wamoja na kuwaletea wananchi maendeleo hivi hebu niulize ujenzi huu
wa barabara ya Lupingu ,Ludewa na Njombe Ludewa unaoendelea ni kwa
faida ya nani hii barabara inatumiwa na wana CCM pekee mbona hata
wapinzani mnapita katika barabara hiyo hiyo sasa unapinga nini
wakati huu wa CCM kutekeleza ilani yake ....tuwe na uzalendo wa nchi
yetu tusiwe wa kupinga kila kitu na mimi nikueleze wazi kama
ungejaribu kupinga mradi huu wa umeme kwa kutoshiriki tungeonana
wabaya mbele ya safari"
Akielezea
mradi huo wa umeme Filikunjombe alisema kuwa kwa kasi ambayo
wananchi wanaenda nayo katika kujitolea nguvu zao kuchimba mashimo
na kusogeza nguzo katika mashimo hayo ni wazi mradi huo wa umeme
utakamilika kabla ya Desemba mwaka huu .
Aidha
alisema kuwa wakati akiingia madarakani mwaka 2010 ni kijiji kimoja
pekee cha jimbo hilo la Ludewa ambacho kilikuwa na umeme wa mafuta
ila sasa zaidi ya vijiji 10 vina umeme na kuwa hadi sasa jumla ya
vijiji 49 vitafikiwa na mradi wa umeme huo ambao unatekelezwa kwa
nguvu za serikali ya Tanzania , Swedeni na kanisa na Romani Katoliki
Dayosisi ya Njombe.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akishiriki kubeba nguzo za umeme wakati wa uhimizaji wa wananchi wa kata ya Lupingu kushiriki maendeleo ya kupeleka umeme kata ya Lupingu |
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishiriki kubeba nguzo |
Vijana wakishirikiana na mbunge wao kubeba nguzo za umeme |
jitihada za kupeleka umeme Lupingu zikionekana |
Mbunge Filikunjombe shimoni na diwani wa TLP wakishiriki kuchimba mashimo ya nguzo za umeme |
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishiriki kuchimba mashimo ya nguzo za umeme pamoja na wananchi wa kata ya Lupingu |
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako