Costa katika moja ya matukio yanayoonesha makali yake |
Diego Costa, leo hii
amekata kiu ya wapenzi na washabiki wa klabu ya Chelsea ya uingereza baada ya
kumwaga wino utakaomkalisha katika klabu hiyo kwa miaka mitano ijayo.
Jose Mourinho alishindwa
kupata kikombe chochote katika msimu wake wa kwanza baada ya kurejea katika
klabu hiyo; Costa ana imani atasaidia kumaliza ukame wa mataji katika klabu
hiyo.
Costa aliyejiunga na klabu hiyo kwa dau
la pauni za Uingereza Milioni 32 akitokea Atletico Madrid ya Hispania anatarajia
kujiunga na kambi ya Chelsea wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako