Hii ni neema nyingine kwa Diamond Platnumz, baada tu ya kuwa verifie
kwenye mtandao wa twiter, hatimaye sasa kuwa Verified kwenye mtandao wa
kijamii wa
Facebook, hii inamaanisha kuwa kampuni ya Facebook hivi sasa
inamtambua Diamond Platnumz kuwa kama msanii maarufu wa kimataifa,
nafasi hii wanatokea kupata wasanii wachache sana na watu maarufu ambao
wanapata bahati ya kujulikana na makampuni makubwa kama haya.
Mwanamitindo wakimataifa Flaviana Matata ni mmoja wa watu maarufu
watokao nchin Tanzania wanaotambuika na kampuni hiyo, na ni moja ya watu
maarufu ambao account yao ipo Verified kama hii ya Diamond Platnumz.
Huu ni mwaka mzuri sana kwa Diamond Platnumz kwa matukio yanayoendelea
kumtokea, na kuzidi kumpa jina kubwa ulimwenguni kupitia muziki wake huu
wa Style yake ya kipekee iliyopewa jina la AfroPop.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako