Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika anatarajiwa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa muda mrefu,mwishoni mwa wiki.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Rais.Taarifa hii iliwasilishwa na msemaji wa
Rais Chikondi Juma aliyesema kuwa sherehe ya harusi itakuwa ya faragha. Rais Mutharika aliibuka mshindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi jana ambapo mshindani wake mkubwa alikuwa rais aliyeondoka mamlakani Joyce Banda.
Rais Mutharika amewaambia maafisa wa serikali kuhakikisha kuwa hakuna pesa za serikali zitatumiwa katika shughuli hiyo.
Baadhi ya wadadisi wanaunga mkono harusi ya Mutharika wakisema kuwa itasaidia kuimarisha maisha ya kijamii na kisiasa kama kiongozi wa nchi.
Hii ni mara ya pili kwa Rais kufanya harusi akiwa mamlakani nchini humo.
Wa kwanza alikuwa Rais Bingu Wa Mutharika,aliyemuoa mpenzi wake Callista Chimombo, aliyekuwa waziri wa zamani wa utalii mwaka 2010.
Wa Mutharika alikuwa nduguye mkubwa rais Peter Mutharika.
Hata hivyo wakosoaji wanalalamika kuwa pesa za umma zitatumika kwa harusi hii kwa sababu shirika la habari la taifa lilatumika kupeperusha matangazo ya harusi hiyo moja kwa moja.
Pia wanasema kuwa Rais Mutharika atatumia rasilimali za serikali ikiwemo usalama wakati wa harusi yake ambayo wanasema bado ni gharama kwa serikali.
BBC
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako