Usiku wa April 13 2014 lililipuka bomu kwenye baa moja Mianzini Arusha na kujeruhi zaidi ya watu 15 wengi wao wakiwa wanatazama mpira ambapo mpaka sasa haijajulikana ni nani alihusika.
Usiku wa May 5 2014 yani jana saa mbili na dakika 20 umetokea mlipuko mwingine ndani ya
kanisa la KKKT Makongoro wilayani Ilemela Mwanza ambao umethibitishwa na Polisi.
Polisi imethibitisha kwamba uchunguzi wa awali umeonyesha bomu hilo ni la kienyeji na baada ya kulipuka limemuathiri mtu mmoja aitwae Bernadetha Alfred kabila Mnyaturu mwenye umri wa miaka 25 ambae kwa sasa anatibiwa kwenye hospitali ya Bugando.
Jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama bado wanaendelea kuchunguza hili tukio manake hata aliefanya shambulio hili pia bado hajajulikana.