A

A

BREAKIN NEWZZZ:- MKE AZIRAI BAADA YA KUHUKUMIWA MIAKA MITANO JELA YEYE NA MUMEWE LIVE

Asia Hamisi akiwa amezirai mahakamani baada ya kuhukumiwa miaka mitano jela.!!



Watu wawili wa familia moja Frank Charles na mkewe Asia Khamis wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi.

Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Mbeya Maria Batulaine amewatia hatiani wanandoa hao baada ya  kuridhishwa na ushahidi usio shaka wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka.

Imedaiwa na Mwendesha mashitaka wa Serikali Juliana William amesema kuwa washitakiwa hao walikutwa na kete 100 za bangi Novemba 19 mwaka jana eneo la Makunguru Jijini Mbeya baada ya upekuzi wa Polisi.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili aliwapa washitakiwa nafasi ya kujitetea ambapo walisema kuwa wana watoto wawili mmoja akiwa darasa la nne na mwingine akiwa kidato cha tatu hivyo kuiomba mahakama kuwaangalia kwa jicho la huruma kwa kuwa hilo ni kosa lao la kwanza.
 

Wakati Hakimu Batulaine akitafakari adhabu kwa washitakiwa hao mshitakia wa pili Asia Khamis alianguka ghafla kizimbani na kuzirai na kumwacha Hakimu akiwa kimya kwa muda kabla ya kutoa hukumu.

Mwendesha mashitaka Juliana William aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya kuvuta na kuuza madawa ya kulevya.

Hakimu Maria Batulaine aliwahukumu kwenda jela miaka mitano jela au kulipa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja na mshitakiwa wa kwanza alikuwa akihaha kutafuta fedha hizo na baadhi ya wasamaria walikuwa wakitoa huduma kwa mkewe baada ya kudondoka kizimbani na  kuzirai.