A

A

Asingefanya haya, Diamond angebaki kuwa underground na tuzo zingebaki kuwa ndoto.


nataka-kulewa3
Una habari kuwa kuna sababu zilizompelekea diamond kuzidi ku-make headlines siku hadi siku?, kama ilivyo kwa msanii yeyote yule mwenye mafanikio duniani, kuna ishu mbili tatu zilizowahi kumtokea katika maisha yake, ambazo ndio zilimpelekea kumsukuma, pamoja na jitihada za kujituma, kuweza kumfikisha hadi kwenye mafanikio yake. Kama ulikuwa hujui, basi bila Diamond kufanya haya, hii leo, hizo tuzo zote, kuanzia ya mtv na kili zingekuwa bado ni ndoto, na kwa hapa Tzee angekuwa na-hit tu kinyumbani nyumbani kama ilivyo kwa wasanii wengi wa bongo fleva.
10012448_682787231779836_1342742437_n
Ugomvi uliompelekea kubadili maisha yake.
Rumors has it kwamba, bila Diamond kugombana na aliyekuwa manager wake wa zamani, hii leo asingekuwa
amefikia hapa alipo, manyanyaso aliyoyapata hapo nyuma, akiwa na uongozi wake wa zamani, ndio iliyomsukuma kufanya vitu kwa bidii na kufikia hadi hii leo, mbali na struggle zake za kila siku katika kujitangaza kimuziki.
1diamond
Inasemekana kuwa management yake ya sasa ndio inayompa sapoti kubwa sana katika kufanya vitu ki-international zaidi, na jina lake kuzidi kukua ulimwenguni, hadi kwa hivi sasa watu wamesha msahau Diamond wa mbagala.

Alipoamua kufaya jambo la hatari katika muziki wake.
Cover
Kama ilivyo katika kila biashara, bila risk huwezi kupata kile ulichokuwa unatarajia, na wala huwezi kuendelea, utabaki hapo hapo siku zote, hii ndio mchezo aliofanya Dangote, kuanzia kutoka kufanya video za milioni mbili hadi kufikia mahali na kufanya video za zaidi ya milioni ishirini, kitendo hichi ndicho kilichopelekea Diamond Platnumz aweze kujulikana zaidi nchi mbali mbali, haswa kwa nyimbo yake ya “my Number1”. Ni moja kati ya vitu ambavyo matunda yake yanaonekana hadi leo, kwa kuendelea kukaa on top kwenye charts, hadi kumpelekea tuzo mbalimbali.
Uchawi wake na mashabiki.
Diamond na Ney wa Mitego jukwaani
Ukitasmini vizuri katika game la hapa Bongo, unaweza kusema Diamond anatumia uchawi, jambo ambalo hata watu wengi wasioelewa faida za kufanya kazi kwa bidii na kujituma ndio zinazomfanya Diamond Platnumz azidi kutoa nyimbo kali kila siku na kuzidi kupendwa na mashabiki wake, kitu kinachopelekea kuwa na u-lukuki wa mashabiki kila siku.Diamond ndiye msanii anayesemakana kuwa na heshima na kuwajali mashabiki wake wa kila rika popote pale alipo,Diamond Platnumz ndiye msanii anayeongoza kuwa na mashabiki wengi zaidi hapa bongo na nje ya mipaka ya Tzee.

VIBE