A

A

STRONG MESEJI KUTOKA KWA BI.JESTINA MERU ON WABONGOZ WOTE HUKO MAJUU NA KUJIFICHAFICHA KWENYE KUJAMIIANA

Kusema ukweli hii inmenisikitisha sana maana inavyo elekea haikuwa matakwa ya marehemu kuchowa lakini kwa kuwa ndo kitu kilicho bei nafuu baada ya kukosa pesa za kumzika basi ndugu yetu apumzike kwa amani.
Lakini pia tujifunze kitu kwa sisi tulioko ugahibuni jamani hakuna kitu kizuri kama kujumuika na watu wako no matter what hata kama si sana lakini fanya mazoea japo uhudhurie mambo ya nchini kwako kama vile misiba na mikutano.
Najua na nimekutana na watu wengi utasikia "mimi wabongo nawakimbi kabisa mara sijui nini" lakini kiukweli no matter what ukiwa na tatizo ndo hao hao wabongo au watu wakwenu watakao kusaidia na
mifano mingi tumeona ukiwemo wa marehemu Mike amabye baada ya kutangaza atachowa walijitokeza watanzania wa huko alikokuwa akiishi kujaribu kusaidia ili asichomwe.

Swali najiuliza how come michango haikufikia wakati mara nyingi na karibia misba yote tunafanikisha kusafirisha hata kuzika ndugu zetu?
Jamani tujifunze kupitia hili. Staki kuhukumu na kusema marehemu hakua na mahusiano na watu maana simfahamu, lakini yawezekana kabisa ni moja wapo ya sababu. Na pia tusisahau nyumbani maana mwisho wa siku ndiko tuliko tokea na wengi ndiko tutakapo rudi tukiwa hai au mabaki yetu