Huu ni mtizamo wangu, na nilimfahamisha Mstahiki meya Jerry Silaa pia: huyu mtu ana bahati sana kwamba ni Meya wa manispaa nchini Tanzania, ambapo ukisahapata uongozi upo huru kufanya lolote lile- baya au zuri, la busara au la kipuuzi- pasi kuchelea matokeo. Laiti huyu mtu angekuwa Meya wa eneo lolote lile hapa
Japo mwanzoni alileta majibu ya dharau baada ya kusoma 'tweets' hizo mbili za mwanzo hapo juu, lakini akakumbana na hasira za wananchi wengi ambao hawakupendezwa na majibu yake. Lakini kwa vile neno 'samahani' halipo kwenye kamusi za wengi wa viongozi wetu, Mstahiki Meya 'aliingia mitini' kimyakimya...na hajaonekana tena huko twitter hadi wakati ninaposti bandiko hili.
Swali la msingi: Hivi Katiba Mpya tunayohangaika kuipata huko Dodoma itaweza kweli kutengeneza mazingira yatakayowawezesha wananchi kuwashughulikia 'wahuni wa kisiasa' (political thugs)? Jeuri kubwa inayowafanya watawala wetu kufanya (including kusema) chochote ni kutochelea matokeo. Na japo Katiba tuliyo nayo sasa ina sheria nzuri tu za kumpatia mwananchi kile anachostahili (kwa maana ya haki zake), tatizo limebaki katika usimamizi wa sheria hizo, na pengine kubwa zaidi, sheria hizo kubaki kama maandiko tu yasiyoheshimiwa. Je Katiba Mpya (laiti ikipatikana) itaheshimiwa?
Finally, ninaamini Mstahiki Meya Silaa nafsi itamsuta na atakatisha ziara yake huko Mwanza na kuungana na wananchi katika harakati za kukabiliana na athari za mafuriko Dar (kwa yeye ni Manisapaa ya Ilala). See, kwenda kumwona mgonjwa hakumaanishi kutamfanya aopone bali kwaonyesha kuwa flani anajali. Kadhalika, tunapokwenda kwenye misiba haimaanishi kuwa tutamfufua marehemu, lakini ile tu kuwafariji wafiwa kunaonyesha kuwa tunajali. Nam ,Meya Slaa akiwa Illa/Dar hatozuiwa athari za mafuriko (au kama alivyosema mwenyewe "hawezi kzuwia mvua") lakini kibanadamu tu anapaswa kuwa na wahanga wa mafuriko (japo yeye ana-pick and choose nani anastahili kuitwa mhanga).
Chanzo:Kulikoni