A

A

EXCLUSIVE: Penny Afunguka na kusema Nipo SINGLE tangu niachane na Diamond, Nikipata mwingine lazima kila mtu ajue

Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa siku zote hawezi kudumu katika penzi la siri.

Penny alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la Ijumaa kuainisha kuwa tangu amwagane na Diamond (Nasibu Abdul) ambaye kila mtu alikuwa anamjua, bado hajabahatika kuwa na mtu mwingine.

“Bado nipo nipo sana na kama ujuavyo, mimi siwezi kuyaficha mapenzi kama nimepata mpenzi wala haichukui muda kila mtu atajua tu,” alisema Penny