Afrika
Kusini ni nchi yenye uchumi mkubwa Afrika ambao umevutia Waafrika wengi
kukimbilia huko kwa ajili ya kufanya kazi kama za Udereva, uuzaji
mafuta kwenye vituo vya mafuta pamoja na kazi nyingine mbalimbali.
Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni kwamba
Watanzania ambao
wanamiliki na kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za Maduka na wale
wanaomiliki hoteli, wamevamiwa wakiwa kwenye mali zao na kufanyiwa
uharibifu na nyingine kuchomwa moto.
Ni kundi la watu ambalo linaendeleza uvamizi huu ambapo linawashutumu
Watanzania hawa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, yani kwa ufupi
Watanzania wanasema hata kama kweli wangekua wanafanya hii biashara,
walio na mamlaka ya kuwavamia ni Polisi na sio hao raia.
Inaaminika
kundi hili lina sehemu kubwa ya madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo ambao
wamekua wakiumizwa na jitihada za raia wa kigeni wa Nigeria na
Watanzania ambao wamejazana kwenye mtaa wao wakimiliki maduka mbalimbali
yakiwemo ya nguo pamoja na hoteli.
Tayari balozi wa Tanzania amekutana na Watanzania hao na kuahidi
kulifatilia ambapo ni Watanzania watano wamejeruhiwa wakiwemo watatu
ambao bado wako hospitali na mmoja wao kavunjika mkono, mmoja kapigwa
kichwani.
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi kufunga maduka yao, maduka matatu
ya Watanzania pamoja na hoteli mbili zinazomilikiwa na Watanzania
zilivamiwa na wakachuchukuliwa simu na watu kupigwa ambapo polisi
walipokuja hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya maelezo.
Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania akiwa anakimbia baada ya kufanikiwa kufunga duka lake.