Baada
ya kutekwa nyara kwa muda wa miaka 3 wakenya wawili waliokua
wakihudumia kwenye shirika moja la Kijamii la kutoa misaada wameachiwa
huru,Wakenya hao ni James Gishoi mwenye miaka 53 na Daniel Wanyoike 25
ambao wamekutana na jamaa na marafiki baada ya kusafirishwa kwa ndege
hadi Nairobi kutoka liboi.
Madereva hao wawili wa shirika la Care International walitekwa nyara
na kuzuiliwa katika Magereza yanayo shikiliwa na wapiganaji hao ambapo
Ilimbidi Daniel wanyoike ajisalimishe ili kuachiliwa kwa wapiganaji hao.
Wawili hao wamesema kwamba uadui kati ya
Al Shabaab na Raia wa Kenya
ulichochewa na hatua ya Kenya kuwapeleka maafisa wake wa jeshi nchini
humo James na Daniel wamesema kwamba wameshuhudia mateka wenzao
wakichinjwa na kupigwa risasi mbele yao kwa miaka yote mitatu Ambayo
wamekua katika gereza la Barahwe ingawa wamekua wakiamishwa kila wakati.
Aidha mateka hao walitembea kilomita 40 magharibi mwa jiji la Barahwe
kuelekea mji wa Dobley ili kukutana na jeshi la Amisom,wakuu wa jeshi
la Kenya KDF wamesema kwamba wataendelea kuwashikilia wawili hao huku
wakipewa ushauri nasaha na kuwahoji ilikupata taarifa zaidi kuhusu
wakenya na Raiya wa nchi zinginezo walio salia kwenye mikono ya
wapiganaji wa al shabaa