MAUZA uza matupu kaburi la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi wa Ilala
katika Manispaa ya Iringa aliyezikwa mwaka jana na leo baba wa
mtoto huyo kakuta chungu cha ajabu chenye damu,maini na kichwa cha
ndege kimechimbiwa kaburini.
Tukio hilo la aina yake limetokea leo majira
ya saa 2 asubuhi katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa wakati
baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Mlawa wakati akichembua kaburi hilo na
mara baada ya kumaliza ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu cha
ajabu kuibuga juu ya kaburi hilo .
" mimi hapa leo nilikuja kusembua kaburi la
mwanangu ila baada ya kumaliza ghafla nilikuta kama damu zinaruka
juu kutoka kaburini na baada ya kuchunguza ndipo nilipoona chungu
hicho kikiibuka huu ya kaburi "
Alisema kuwa chungu hicho kilikuwa
kimefungukwa na kitambaa cheusi juu ambacho kimelowa dawa na
kufungwa kamba ya nguo ya kijani na kutokana na tukio hilo la ajabu
alilazimika kuacha jembe juu ya kaburi na kukimbia kuita watu
wanaopita barabarani ili kuomba msaada zaidi.
Mzazi huyo anadai kuwa mazingira ya kifo cha
mtoto wake yalikuwa ni ya kushangaza baada ya kuugua kwa muda wa
siku nne pekee na kufariki dunia .
Hata hivyo alisema kwa kuwa kwa upande wake
haamini mambo ya kishirikiana hakuona sababu ya kumwita mganga wa
kienyeji kwa ajili ya kushughulikia kuchoma chungu hicho na badala
yake kuamua kuifanya kazi hiyo mwenyewe hasa akiamini nguvu ya
Mungu zaidi.
" Napenda kuwashukuru wananchi waliofika hapa
kwa kunitia nguvu na pia kuwashukuru madereva boda boda akiwemo
kijana Ahmed kwa kujitolea mafuta ya Petrol kwa ajili ya kukichoma
chungu hiki "
Mbali ya mzazi huyo kujitolea kuchuma chungu
hicho na kuteketeza vitu vilivyo kuwemo ndani wananchi waliofika
kushuhudia tukio hilo walilazimika kutimua mbio kuhofu zoezi hilo
la uchomaji wa tunguli hizo. |