Kiungo
wa zamani wa Arsenal na Real Madrid anayekipiga katika klabu ya
Lokomotiv Moscow Lassana Diarra amekanusha madai kwamba ni mfuasi wa
vita ya kidini nchini Syria.
Wiki iliyopita iliripotiwa kwamba Diarra (29) alijiunga na vita
inayoendelea Syria baada ya kutolewa kwa video inayomuonyesha mtu akiwa
kajifunika uso huku akijitambulisha kwamba ni Lassana Diarra.
Hata hivyo kiungo huyu wa timu ya taifa ya Ufaransa ambae aliwahi pia
kuitumikia Portsmouth na Chelsea, ametoa taarifa rasmi kupitia wakili
wake na kusema hahusiki kabisa na hiyo video.
“Hajawahi kukanyaga nchini Syria, ni ujinga na yeye sio mfuasi wa
jihad, ni mwanasoka anayeichezea Lokomotiv Moscow,” amesema Mwanasheria
wake.