A

A

Ray C alipowatembelea Wahanga wa Madawa ya Kulevya huko Kigamboni,Ibra da Hustler yumo

Rehema Chalamila ‘Ray C’ baada ya mchakato wakutafuta logo kwa ajili ya foundation yake ya kupambana na kusaidia vijana wasiingie kwenye matumizi ya dawa za kulevya hatimaye ameanza kazi. 

Ray C ametembelea kituo cha vijana walioamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na tabia hatarishi huko Kigamboni ambapo kwenye kituo hicho Ray C alikutana na msanii aliyekua wa Nako II Nako Ibra Da Hustler.

Ibra yupo kwenye kituo hicho na vijana wengine walioachana matumizi ya dawa za kulevya ambapo Ray C amemuhoji hivyo hiyo interview itaonekana kwenye program inayoandaliwa na foundation yake. 



 



 



Ibra akiwa na Ray C.