Kamanda
wa kanda maalum ya Dar es salaam Kamishina Suleman Kova akizungumza
na wanahabari muda huu ofisini kwake juu ya kufukuzwa kwa askari hao.
Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewafukuza kazi kwa fedheha askari wanne wa
Jeshi la Polisi kutokana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Askari waliofukuzwa wanatoka katika vikosi mbalimbali kama ifuatavyo:
E.6396 CPL
RAJABU MKWENDA @ UGORO wa Makao Makuu ya Polisi.
· F.9412 PC SIMON
wa Kituo cha Polisi Kati.
· F.9414 PC
ALBERNUS KOOSA wa Kikosi cha Bendi ya
Polisi D’Salaam
· F.9512 PC
SELEMAN wa Kituo cha Polisi Kigamboni
Uchunguzi wa
awali umeonyesha kwamba askari hao wamekuwa wakijihusisha na uhalifu ikiwa ni
pamoja na tukio la tarehe 09/03/2014 eneo la Mbezi Beach “A” ambapo majambazi
wapatao 15 walifika katika ofisi ya
Kampuni ya Kichina ijulikanayo kwa jina la HONG
YANG inayojishughulisha na
ujenzi na uselemala.
Katika tukio
hilo majambazi wapatao 11 wakivamia ofisi hiyo majira ya saa 04:30 Asb, na
kupora vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslim, simu, n.k. na kutoweka.
Imegundulika
kwamba baadhi ya majambazi hai ni askari Polisi. Uchunguzi wa kina umefanyika na watuhumiwa hao 11 wamepatikana
ndipo ilipobainika kwamba askari Polisi hao walishiriki katika tukio hilo.
Watuhumiwa
wengine saba wa ujambazi waliokamatwa ni hawa wafuatao:
· GERADI S/O
RAJABU MTUTU, Miaka 36, Mfanya biashara, mkazi wa Mtoni Mtongani.
· CHARLES S/O HIZA
MBELWA, Miaka 37, Fundi magari, Mkazi wa Kurasini.
· ADAM S/O
MKOMBIZI MOHAMED, Miaka 40, Mkazi wa Kariakoo.
· ALLY S/O RASHID
SALUM, Miaka 38, Mkazi wa Vingunguti Spenco.
· SALUM S/O ABDUL
MUSSA, Miaka 22, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbagala Kuu.
· JUMA S/O SAID
HAMIS, Miaka 29, Mkazi wa Yombo kwa Limboa.
· JUMA S/O OMARI
NGWELE, Miaka 50, Mfanyabiashara Samaki Ferry, Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.
Watuhumiwa wote
hao wametambuliwa na mashahidi mbalimbambali katika tukio hilo. Kabla ya
kufukuzwa kazi, askari hao walishtakiwa katika mahakama ya kijeshi na
walipatikana na hatia hivyo wamepewa adhabu ya kufukuzwa kazi kwa kosa la
kulifedhehesha Jeshi la Polisi. wamefukuzwa kazi kuanzia tarehe 17/03/2014 na
sasa si askari tena bali ni raia wa kawaida.
Aidha jalada la
kesi hiyo pamoja na majalada mengine ya kesi ya wenzao waliowataja yatapelekwa
kwa mwanasheria wa Serikali hivi karibuni kabla ya kuwafikisha mahakamani kwa
makosa jinai.
Pamoja na malezo
hayo, Jeshi la Polisi halitavumilia vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya
utumishi wa Jeshi la Polisi na hatua hizi ni fundisho kwa askari wa cheo chochote
atakayejaribu kwenda kinyume cha taratibu na maadili ya kazi.
Jeshi la Polisi
litaendelea kuwazawadia askari wenye kufanya vitendo vya ujasiri vinavyoendena
na tabia njema kama ilivyofanyika hivi karibuni tarehe 07/03/2014. Pia Jeshi la
Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu maafisa, wakaguzi na
askari watakaokiuka maadili au kukiuka mwenendo mwema wa Jeshi la Polis
|