Sasa jingine jipya kwa sasa ni kuhusu Rais Uhuru kuagiza wakuu wote
wa mashirika ya serikali nchini Kenya kupunguzwa mshahara kwa asilimia
20 na
kwamba watakaopuuza agizo hilo watafutwa kazi ili nafasi hizo
wapewe wengine walio tayari kupokea mshahara wa chini.
Namkariri akisema ‘Nakuhakikishia kuna Wakenya wengi wako tayari
kuchukua hizo nafasi kwa mshahara huohuo mdogo, watakaogoma kupunguzwa
mshahara waondoke waende Mahakamani ambako hata wakishinda itakua rahisi
sisi kulipa fidia na kupata watu wengine hivyo wasidhani wataturudisha
nyumba kwa kwenda Mahakamani’
‘Kama huwezi kukubali nenda utafute pahali ambapo wako tayari
kukulipa huo mshahara na hiki ni kitu ambacho kitaendelea kufanyika
kwenye sehemu zote, na niwakumbushe tu kwamba hatufanyi hivi kwa ajili
ya kumuumiza yeyote’ – Uhuru Kenyatta
Wakati huohuo Chama cha ODM kimepinga vikali hili agizo la Rais
Kenyatta la kulazimisha wafanyakazi wa Serikali kukubali mshahara wao
kupunguzwa na kwamba Rais na Naibu wake ni wanafiki.
ODM wanasema wawili hawa hawana majukumu ya kulipa kodi ya nyumba au
nauli miongoni mwa majukumu mengine huku marupurupu wanayopokea yakiwa
makubwa bado hivyo kukatwa asilimia 20 ya mshahara wao haitosaidia
kuboresha maisha ya Wananchi.
Hii ishu umeionaje?
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako