Matumizi hayo mabaya ya madaraka yanadaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7 kwa kutoa msamaha wa kodi.
Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Jaji John Utamwa baada ya
washtakiwa hao kuwasilisha maombi ya kwenda kutibiwa nje ya nchi ambapo
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na maombi hayo.
Baada ya kusikiliza ombi hilo Jaji Utamwa alisema
mahakama
inawaruhusu washtakiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kutibiwa na kwamba
pamoja na ruhusa hiyo amewataka Mramba na Yona kuwepo mahakamani siku ya
kusikiliza kesi hiyo Aprili 22 mwaka huu.
Katika kesi hiyo inayowakabili Mramba na Yona piamshtakiwa mwingine
ni Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha Gray Mgonja,Kesi hiyo
imepangwa kusikilizwa Aprili 22 hadi 25, mwaka huu.
Katika kesi ya msingi washtakiwa wanadaiwa kuwa kati ya Agosti mwaka
2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam wakiwa watumishi wa umma
kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.
Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya
Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia
kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business
Corporation waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini
ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.
Source:issamichuzi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako