Viongozi wa CORD nchini Kenya wamewataka wabunge wake kuimarisha juhudi zao kama chama cha upinzani na kufanya mabadiliko muhimu katika muelekeo wa nchi kwa wakati huu.
Viongozi wa CORD walikutana na wabunge na masenta katika mji wa Naivasha kwa mazungumzo ya siku mbili kujadili ajenda yao kuhusiana na masuala ya kuimarisha mfumo wa Ugatuzi, mabadiliko ya katiba, ufisadi na ulaji rushwa, pamoja na ugaidi nchini Kenya.
Akizungumza na Sauti ya
Amerika Moses Wetangula , moja wapo wa viongozi wa tatu wa mungano huo amesema wamezungumza na wabunge wao 129 na kuwapa muongozo wa chama watakapofungua bunge wiki hii.
Bw. Wetangula aliyekuwa waziri wa
zamani wa mambo ya nchi za nje anasema, "CORD ni muungano wenye nguvu ,
uloimarishwa na unamuelekeo unoaofaa, kwa sababu viongozi wake Raila
Odinga, Kalonzo Musyoka na mimi tumekubaliana ya kwamba miungano
inayoundwa kwa haraka kwa ajili ya uchaguzi haidumu. Sisis tunataka
muungano wetu uwe wa kudumu na mfano Kenya"
Akizungumza na waandishi habari
kiongozi wa CORD Bw. Odinga, ametoa wito kwa wabunge wake kuwaondowa
wajumbe wa tume ya uchaguzi akidai kwamba walishindwa katika uchaguzi
ulopita kwa ajili ya uzembe wao katika kazi.
Wakati viongozi wa CORD walikua
wanakutana Naivasha viongozi wa Jubilee walikutaka kwa mkutano wa
faragha katika Ikulu ya Nairobi kujadili pia mikakati yao kabla ya
kufunguliwa bunge.
Chanzo, voaswahili.com
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako