Dar es Salaam, 5 Februari,
2014.Tunapenda kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa kushindwa kutoa
huduma za mawasiliano kuanzia asubuhi ya Februari 5, 2014. Hii
imetokana na kukatika kwa mkonga wa mawasiliano ulioko barabara ya
Morogoro na nyingine mbili za ziada zilizoko Mlalakuwa na Mayfair plaza
barabara ya Mwai kibaki jijini Dar es Salaam.
Kukatika kwa Mkonga huo kumesababisha
vituo vyetu vya kutoa huduma za mawasiliano vilivyopo Oysterbay na mbezi
juu kushindwa kufanya kazi kutokana na vituo hivyo kutegemeana
kumesababisha kushindwa kutoa huduma za mawasiliano.
Kutokana na hilo wateja hawakuwa na
uwezo wa kupiga simu, kutumia intaneti na hata huduma za kifedha.
Tunatambua usumbufu ambao umetokea kwa kukosa mawasiliano, kwa mara
nyingine tena tunaomba radhi na tunashukuru kwa uvumilivu wao katika
kipindi chote ambacho huduma zilikosekana.
Mafundi wetu wameweza kurekebisha
uharibifu uliotokea barabara ya Mwai kibaki ambao uliotokana na shughuli
za ujenzi wa barabara zinazoendelea. Uharibifu mwingine uliotokea
katika Barabara ya Mlalakuwa ulichukua muda kurekebisha kutokana na
nyaya zilizo katika mkonga wa mawasiliano kuungua kulikosababishwa na
zoezi la uchomaji taka lililokuwa linaendelea katika sehemu ambayo
mkongo umepita na kusababisha uharibifu huo.
Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa,
Tumejidhatiti katika kuendelea kutoa huduma bora na za kipekee wakati
wote watakapokuwa wanautumia mtandao wa Vodacom, Tunawashukuru kwa namna
ambavyo wameendelea kutuunga mkono na kutuvumilia pale matatizo
yanapojitokeza.
Rene Meza
Mkurugenzi Mtendaji – Vodacom Tanzania

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako