Siku
kadhaa zilizopita kupitia millardayo.com kuna taarifa ziliztoka kuhusu
kufungiwa kwa video ya Nimevurugwa ya Snura,taaarifa hizi alizi-amplify
meneja wake Snura ‘Hk’ akidai kuwa sababu maalum bado hawajazipata
ingawa kila kituo anachoenda wanampa sababu tofauti. moja kwa moja kwenye Baraza la
Sanaa la Taifa(Basata)ili kuujua undani wa sakata hili ikiwemo pia
kuulizia video ya Jux(uzuri wako)ambayo nayo ilitoka taarifa ya
kufungiwa kwa video hiyo.
Kutoka Basata huyu hapa Godfrey mungeleza ni
kaimu katibu mtendaji
anataarifa zaidi>>Unaposema kufungia video moja kwa moja kuna
chombo kingine cha serikali kinashughulikia hilo ambao ni bodi ya filamu
Tanzania’
‘Bodi ya filamu wanaangalia video zote suala zima la filamu wanapoona
hii haikidhi au haifai kwa jamii za Kitanzania basi wanaisimamisha
kidogo wanamshauri aweze kuirekebisha ili iweze kulingana na maadili ya
kitanzania’
‘Sisi tunaangalia Audio kabla haijaingia sokoni katika urasimishaji
tunakaa tunausikiliza muziki wake tunashauriana kwamba akarekebishe hapa
na tunaangalia mambo mengi ikiwemo ubunifu wake mwenyewe’
‘Suala la kufungiwa kwa Snura najua kabisa linaenda kwenye suala la
maadili na limeandikwa sana na sisi Baraza kama Baraza tunaangalia sana
suala la maadili tukisema tunamfungia hatufungii video tu tunamfungia
msanii mwenyewe’
Bonyeza play kumsikiliza Kaimu Katibu mkuu akielezea suala hili.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako