Joshua Nassa ajitambua,Akaa Upande wa Wananchi Swala la Posho za Wabunge
MSIMAMO WANGU, SAKATA LA POSHO BUNGENI.
Nimeona nukuu kwenye gazeti la nipashe la leo. Kimsingi ike nukuu si ya
kwangu ni nineshazungumza na Mhariri wa jipashe Bw. Kwayu.
Sijui kama nukuu ile imewekwa kwa kukosea au kwa makusudi, wameahidi
kurekebisha makosa lakini ni vyema nikaweka msimamo wangu hapa.
Kwa hali halisi ya maisha ya kawaida ya Mtanzania wa shilingi laki 3 ni
fedha nyingi. Na taasisi ya Bunge ndiyo inayopaswa kuwapigania hawa
watanzania ili vipato vyao vipande lakini taasisi hii siku zote
imekubali kuwa upande wa serikali badala ya kuisimamia serikali kwa
niaba ya wananchi.
Fedha hiyo bado ni nyingi mno kama kipato cha mtanzania kinabaki kuwa hapo kilipo.
Kabla ya kupigania ongezeko ambalo linaweza wakati mwingine likawa na
mantiki, ni vyema wabunge wakaifanya kwanza kazi yao ya kupigania
maisha bora na maslahi bora kwa wananchi hiki hiyo mantiki yao kama ya
kufanya mabadiliko ya posho ya shilingi elfu arobaini 40,000/=
atakayolipwa mbunge iwapo ataugua akiwa Dodoma iweze kuonekana.
Otherwise na sisi wabunge tutakuwa ni sehemu ya dhambi ya mateso na hali
ngumu ya maisha ya watanzania ambao bado wanajifungulia sakafuni na
hawana maji safi ya kunywa.
Joshua Nassari (MB) na mjumbe wa bunge maalum la katiba.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako