Kwenye
kumbukumbu miaka minne iliyopita mshambuliaji toka Tanzania
anayeichezea Tp Mazembe ya DR Congo Mbwana Ally Samatta hakuwahi kumake
headline katika soka hapa nyumbani zaidi ya kusikika kwa mbali wakati
akiitumikia timu yake ya African Lyon.
Msimu mmoja tu baada ya kushiriki Ligi Kuu Bara Dewji aliamua kuiuza
timu hiyo na baadaye Samatta alijiunga na club ya Simba ambayo
aliitumikia kwa msimu mmoja tu kabla ya kuuzwa TP Mazembe ya DR Congo.
Unaambiwa kwa sasa Samatta ni mmoja kati ya wachezaji ghali barani
Afrika na ndiye anayesemekana kulipwa vizuri kuliko wachezaji wengine
wanaocheza soka kutoka Tanzania bila ya kujali wako bara la Afrika,Asia
au Ulaya.
Kwa sasa Mshahara wa Samatta na TP Mazembe kwa mwezi ni dola 10,000
kwa Tanzania ni zaidi ya Sh milioni 16 maana yake mshahara wake unaweza
kuwalipa wachezaji wa timu moja ya Ligi Kuu Bara kwa mwezi.
Mfano ni timu za jeshi kama JKT Ruvu,Ruvu Shooting,JKT Oljoro na
nyinginezo,lakini timu kama Ashanti ni kati ya zile ambazo mshahara wa
mwezi wa Samatta unaweza kuwalipa wachezaji wao kwa asilimia 90 au 100
kabisa.
Lakini mshahara pekee hautoshi kuonyesha mabadiliko ya haraka sana ya
Samatta, vitu vingine vikubwa viwili ni thamani anayopewa kwa kipindi
hiki kuwa imefikia dola pauni 450,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.2).
Taarifa ikifikie kuwa hakuna mchezaji wa Tanzania ambaye aliwekwa
kwenye soko kupitia mitandao maarufu ya mauzo ya wanasoka na akafikia
thamani ya Samatta na ili kuonyesha kuwa thamani yake,Klabu ya Al Ain
inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu ((UAE)unaambiwa iko tayari
kutoa dola milioni 1 (zaidi ya Sh bilioni 1.6) ili kumnasa Samatta
akacheze kwenye timu yao.
Source:Salehjembe.blogspot.com

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako