Mwamuzi aliyechezesha mchezo wa ligi kuu ya Hispania kati ya
Athetico Bilbao VS Real Madrid na kumtoa kwa kadi nyekundu mwanasoka
bora wa
dunia Cristiano Ronaldo wikiendi iliyopita amesimamishwa.
Kamati ya marefa nchini Spain imemuadhibu refa Miguel Angel
Ayza Gamez kwa kumsimamisha kwa mwenzi mzima na huku akiondolewa katika
isti ya marefa watakaochezesha mechi za Real Madrid zilizobakia msimu
huu.
Refa huyo alitoa kadi nyekundu kwa Ronaldo ambayo ilionekana
kuwa na utata mkubwa jambo lilopelekea malalmiko kutoka kwa klabu ya
Real Madrid.
Kutokana na kadi hiyo nyekundu ya moja kwa moja Ronaldo
amefungiwa kucheza mechi tatu na atazikosa mechi tatu zijazo za timu
yake dhidi ya Villarreal, Getafe na Elche.
Hata hivyo kufungiwa kwa refa huyo aliyemsababishia kufungiwa huko
kunaweza kuipa nguvu Real Madrid kukata rufaa dhidi ya kadi hiyo ya
Ronaldo.

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako