Vigogo wa
TBA, Makumba Kimweri (kulia) na Richard Maliyaga (kushoto) wakiwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar! (Picha na Maktaba).
***********
Watu
wawili wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 15 au kwenda jela
miaka miaka 15 baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano ya ujenzi
wa jengo la ghorofa 18 lililojengwa jirani na Ikulu lililopo mtaa wa
Chimala Kitalu cha 45 na 46, kinyume cha sheria.
Washtakiwa
hao ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),
Makumba Kimweri na aliyekuwa Msanifu Mkuu wake Richard Maliyaga (55)
wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi
uliotolewa na upande wa mashitaka dhidi ya washtakiwa, mahakama imeona
wana hatia kwa makosa yote matano.
Alisema
hati ya mashitaka inaonyesha mshtakiwa wa kwanza anakabiliwa na
mashitaka watatu na upande wa mashitaka umethibitisha kweli alitenda
makosa hayo na mahakama inamhukumu kulipa faini ya Sh. Milioni 3 kwa
kila kosa au kulipa faini ya Sh. Milioni 3 kwa kila kosa.
Kwa
upande wa mshtakiwa wa pili, hakimu alisema hakuna ubishi bila kuacha
shaka mshtakiwa, alitenda makosa hayo na kwamba atalipa faini ya Sh.
Milioni 3 kila kosa au kulipa fani ya Sh. Milioni 3 kila kosa.
Hata hivyo, walilipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Katika
kesi ya msingi, washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matano ya
matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji kibali cha ujenzi wa jengo la
ghorofa 15 kiwanja namba 45 mtaa wa Chimara.
Ilidaiwa
kuwa Kimweri alikuwa na wadhifa huo TBA kuanzia mwaka 2002 hadi 2010 na
Maliyaga aliajiriwa mwaka 2002 akiwa msanifu mkuu.
Mwendesha
Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai
alidai kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na TBA, ambako hadi mwaka
2006 kilikuwa hakijaendelezwa.
Aidha
TBA, kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma iliwaalika wanaotaka
kuwekeza kuwasilisha andiko la awali kwa ajili ya uendelezaji.
Wote wamelipa faini na kuachiwa huru
Wote wamelipa faini na kuachiwa huru
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako