JESHI LA AUSTRALIA LAKAMATA MADAWA YA KULEVYA PWANI YA TANZANIA
Askari wa HMAS Melbourne wakiwa na
madawa yaliyokamatwa
JESHI
la majini la Australia limekamata na kuharibu kilo 353 za madawa ya
kulevya aina ya heroin yenye thamani inayokadiriwa kuwa zaidi ya dola
milioni 700 katika pwani ya Tanzania.
Askari wa meli ya HMAS Melbourne waliyagundua madawa hayo katika meli
moja Jumatano iliyopita wakiwa katika shughuli za kupiga vita ugaidi na
kuimarisha usalama maeneo ya baharini Mashariki ya Kati na Bahari ya
Hindi.
Mkuu wa kikosi hicho, Daryl Bates, alisema hatua hiyo ilikuwa ni pigo
katika kukwamisha njia za kupatikana kwa fedha zinazotumiwa na magaidi.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako