A

A

CCM ni Serikali Mbili tu,Wasimama Kidete kama alivyofanya Baba wa Taifa.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kuwa hakitishwi na tambo la vyama vya upinzani kuhusu hatua yao ya kwenda kushitaki kwa wananchi juu ya muundo wa Serikali mbili.
Tamko hilo la CCM limekuja siku chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza uamuzi wake wa kwenda kushitakiwa kwa wananchi ikiwa msimamo wa CCM wa Serikali mbili utapitishwa katika Bunge 
la Katiba.
Kauli hiyo ilitolewa  Mjini Dodoma jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kikao cha Halmashauri (NEC) kilichomalizika juzi mjini hapa.
Alisema CCM haitishiki na wanaotaka kwenda kushitaki kwa wananchi kuhusu msimamo wao wa kutaka kuwepo kwa Serikali mbili.
“Wanaotaka kwenda kushtaki kwa wananchi waende tutawafuata nyuma na majibu, hii habari ya kutishiana tutaenda kwa wananchi kwani mwananchi huyo ni nani.
“Kama wao wanauwezo wa kufika kwao na kujenga hoja na sisi tunao uwezo wa kufika kwao na kujenga hoja, nasema watangulie kwa wananchi tutawakuta huko na tutatoa majibu na wananchi watatuelewa.
“Kama ambavyo wamekuwa wakituelewa kwa kipindi cha miaka 50, wanatuamini tuendeele kuongoza nchi hii ndivyo watatuelewa katika suala la katiba, 
“Tusifike mahali pa kutishia, tusifike mahali pakutaka kuburuzana sio sawa ni akili  ni akili finyu,” alisema Nape
Akizungumzia kikao hicho cha NEC kilichomalizika juzi, Nape alisema kilikuwa na ajenda moja tu ya kujadili rasimu ya pili ya katiba na kwamba rasimu hiyo ilijadiliwa kifungu kwa kifungu.
Alisema pamoja na mambo mengine msimamo wa CCM bado ni uleule wa Serikali mbili na kwamba walichojadili ni maboresho ambayo yanahitajika katika mfumo huo.
“Mapendekezo yetu ni kuwepo kwa Serikali mbili zilizofanyiwa maboresho ambayo ndiyo yatajibu changamoto za mfumo huu kwa sasa na mapendekezo yetu tutayasilisha kwa wabunge wa Bunge la Katiba,” alisema Nape
Alitaka vyama vingine visiweke mazingira ya ugomvi kutokana na msimamo huo wa CCM bali wajenge hoja zao kwa kile wanachokisimamia.

“Kila watu wanamaoni yao wala sio ugomvi, watu washindane kwa hoja na hakuna suala la nani kashinda au nani kashindwa,” alisema Nape

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako