Naibu Katibu Mkuu CCM
Tanzania Bara Mh;Mwigulu Nchemba ameshawasili Jijini Arusha Mchana huu
akitokea Kiteto na Babati kwaajili ya Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani
zinazoendelea nchi nzima,Chaguzi hizi ni ndogo kwaajili ya kujaza nafasi
za Madiwani waliojiuzulu na wengine kufariki.
Naibu
Katibu Mkuu CCM Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Mgombea wa
Udiwani Kata ya Sombetini WIlaya ya Arusha ndugu David,Hapa akiwa kwenye
maandamano kutokea Ofisi za chama hapa Sombetini kuelekea Viwanja vya
Mkutano,Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.
Mh:mwigulu
Nchemba akipata mapokezi mazito kutoka kwa maelfu ya wananchi
waliomiminika Viwanja hivi vya Soko la Mbauda kwaajili ya Mkutano wa
hadhara wa kampeni za Udiwani.
Mapokezi yanaendelea hapa Soko la Mbauda kwaajili ya kuanza mkutano wa hadhara.
Sehemu
ya Mamia ya Wananchi wakiwa tayari kusikiliza Mkutano huu wa hadhara
kwaajili ya Kampeni za Udiwani kata ya Sombetini jijini Arusha.
Wananchi
wanaendela kumiminika kwenye viwanja hivi vya soko la Mbauda kwenye
Mkutano wa Hadhara wa CCM kumnadi mgombea wa CCM kwenye Kinyang'anyiro
cha Udiwani.
Mh;Mwigulu Nchemba akionesha Kadi ya Chadema baada ya Wanachama 4 wa CHADEMA kurudisha kadi zao na kujiunga na CCM.
Watu ni wengi sana waliojitokeza kwenye Mkutano huu wa hadhara wa Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Sombetini
Maelfu
ya Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa Hadhara wa Ufunguzi wa
kampeni Kata ya sombetini Jijini Arusha.Mh;MWigulu yupo jukwaani
anawahutubia wananchi sera za Chama cha Mapinduzi na namna CCM
ilivyotekeleza Ilani yake ndani ya kata ya sombetini na namna
Inavyohitaji Diwani wa CCM kuendelea kusimamia Ilani ya Maendeleo ndani
ya kata hiyo.
CCM
imerejesha Heshima yake Jiji la Arusha,Wananchi hawataki tena CHADEMA
kutokana na Vurugu mbalimbali zinazoratibiwa na Chama hicho,Wastani wa
Kufanya Vurugu ndani ya Jiji la Arusha chini ya Chadema ni Mkubwa kuliko
Wastani wa Kufanya kazi za maendeleo kwa Wananchi wa Arusha.
Mh;Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa CCM Mwl.David Mollel mbeye ya Umati wa Wananchi/wakazi wa Sombetini
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba akiwaonesha Wananchi namna
Kijana mwenzao alivyovamiwa na Vijana wanaosadikika ni Wachadema na
Kupigwa hadi kupoteza Fahamu na Kisha kuporwa pikipiki yake pamoja na
Bendera ya Chama Cha Mapinduzi.Mwigulu alisisitiza kwa Kusema
inasikitisha sana kuona Kuna watu wanakiunga mkono Chadema wakati ni
chama kinachoongoza kwa Kuratibu mauaji ya Watanzania wasio na hatia kwa
madhumuni ya kupata Fedha kwa Wafadhili wao nje ya Nchi.
Mkutano
umemalizika hapa Sombetini na Naibu Katibu Mkuu anagana na Wananchi
waliojitokeza kwa wingi kwenye Ufunguzi huu wa Kampeni za Udiwani kata
ya sombetini.
Sehemu
ya Mamia ya Wananchi waliomiminika kwenye uwanja wa Soko hapa
Sombetini wakisikiliza kwa makini Sera za Chama Cha Mapinduzi kutoka kwa
Mh;Mwigulu Nchemba
Picha zote na HABARI KWANZA BLOG
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako