Mwenyekiti wenu,Nawaza tu "YA TANESCO NA ZIGO LA SERIKALI TATU"
NAWAZA TU TANESCO NA ZIGO LA SERIKALI TATU.
TANESCO wameshafanya yao(umeme umekatika)!!!Umeme wenyewe umeshapanda
bei,gharama(Tsh.elfu 10 unapata Unit 8 tu).Licha ya Gharama kupanda,Mgao
ndio kwanza unaonekana kurejea Kwa kasi.Ni maumivu Juu ya Maumivu.
Nadhani tukifanya SENSA ya Haraka tu,Wapangaji wengi
wanakorofishana,kununiana,kupangiana vitu vya kutumia umeme kwa kipindi
hiki kwa kasi kubwa kuliko miaka yote tokea Tanzania iwe Tanzania.
MNAOSHABIKIA SERIKALI TATU,Hii hali ya Kupanda kwa Bei ya Vitu itakuwa mara mbili(Tutalia na Kusaga meno).
Bajeti ya Serikali hiii tuliyonayo ni yakuungaunga/mara kadhaa tumeona serikali ikitafuta fedha za kujazilizia bajeti,sehemu kubwa ya bajeti inatoka kwa watu wanaotusaidia.
Sasa mnataka muongeze ya Tatu,Hiyo serikali ya Tatu Bajeti yake
itapatikana kwa Njia ya Kodi,Hivyp mtegemee Kupanda Gharama za Maisha
maradufu.
Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano bajeti zake
zitakuwa sawa kutokana na ukubwa wa Territory,Ukubwa wa Wizara na Ofisi
ya Waziri Mkuu.Zanzibar wao Mapato yao kwa mwaka ni Billion 150 na
Matumizi yao Kwa Mwaka yanakwenda Billion 300.
SASA Hao Wazanzibary
Watahangaika na Serikali ya Muungano ya nini wakati mapato yao ndio
hayo,Hata sasa kwenye Serikali Mbili Zanzibar hawachangii chochote
kuendesha serikali ya Muungano(Tanganyika ndio kila kitu).
Narudia
tena Serikali Tatu ni Mzigo kwa Nchi.TUPINGE VIKALI
Wanaoipendekeza(Rejea Warioba alisema TUME INAPENDEKEZA MUUNDO WA
SERIKALI TATU) hawajawahi ishi ndani ya serikali hiyo,na
hawanachakupoteza na Serikali Tatu zitaleta Mzigo kwetu vijana na sio
rika la waliopendekeza.
KAma wewe unaona kwasababu CCM ndio
inapendekeza serikali mbili,Basi kwa Ujinga wako wa kupinga kila kitu
cha CCM unapinga na hili bila kufikiria kuwa Kodi itakapopanda hapa
haitakuwa kwa WanaCCM tu ni Kwa Watanzania wote.
Note:SWALA LA
KUVUNJIKA KWA MUUNGANO SI KWA SABABU YA MFUMO WA SERIKALI,NI DHAMIRA YA
WAHAFIDHINA WACHACHE WANAODHANI ZANZIBAR IKIJITENGA ITABAKI SALAMA,AU
ITATAJIRIKA SANA,WANASAHAU UPEMBA NA UUNGUJA ULIOFICHWA NA HUU MUUNGANO
TULIO NAO.
Tafadhali usininukuu