Unaweza kudhani ni simulizi za kale,.
Huwezi kuamini kuwa ni ndani ya Jiji la
Dar es salaam ambapo wakazi wa mtaa wa Karakata hulazimika kufunga
biashara zao na kujifungia majumbani mwao ili kuokoa maisha yao yasije
yakalaruliwa na MBWA MWITU "WATU" wanarandaranda mitaani wakiwa na
silaha za jadi (mapanga, fimbo, magongo na nondo) na kupora mali na
kudhuru mwili kwa kila watakayekutana naye mida ya jioni hadi usiku wa
manane.
Vijana hawa wanaotembea katika makundi ya watu wasiopungua ishirini wakikutana na raia hupora hata nguo za mwilin! Sijui
serikali iko likizo ama nayo ni sehemu ya mchezo? Maana kata hii ndiyo
yenye kituo kikuu cha polisi cha wilaya ya Ukonga - Sitakish