Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amekiri Serikali kuwa katika hali ngumu,
lakini akasema kuwa mkakati uliopo ni kudhibiti matumizi ili yaendane na
fedha iliyopo.
Waziri Saada alisema hayo kwa njia ya simu, alipotakiwa na Mwananchi
Jumapili kujibu madai ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) juu
ya kauli yake ya hivi karibuni aliyoitoa katika mkutano mjini Dodoma.
“Ni kweli nimesikia alichosema CAG na nadhani alimaanisha kudhibiti
matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji. Siyo kwa Tanzania tu, nchi
zote huwa zinazingatia matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji
yaliyopo” alisema Saada na kuongeza:
“Sisi kama wizara tumejipanga kukusanya na kutegemea fedha zetu za ndani
kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA). Tunategemea misaada, lakini huwa
inachelewa. Hata wakaguzi nao wanapaswa kuangalia hilo.”
Hata hivyo, Saada alisema kuwa Serikali ina fedha za kutosha kuendesha shughuli zake.
Alhamisi wiki hii CAG,Ludovick Utoh akifungua Mkutano wa pili wa Baraza
la Wafanyakazi wa Ukaguzi nchini mjini Dodoma alisema, Serikali ya
Tanzania iko hoi kifedha hivyo Bunge na Serikali lazima wajitathimini na
kuongeza wanayo matumaini kutokana na ushauri ambao umekuwa ukitolewa
na ofisi yake kufanyiwa kazi.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako