A

A

Taarifa Mbaya tulizopokea Usiku huu ni Kifo cha Msanii huyu wa Twanga Pepeta

mcd 
AKama mfatiliaji wa muziki wa Dansi Tanzania,jina la Mc D si jina geni kwako,jina lake halisi ni Masoud Mohamed,ni mpiga tumba kutoka bendi ya African Stars Band’Twanga pepeta’ taarifa hizi zimetangazwa usiku huu na kuthibitishwa na msemaji wa Twanga pepeta Hassan Rehani .
Taarifa zaidi inasema kuwa Mc D alikua yukoMoshi kwa ajili ya matibabu zaidi ya miezi miwili na hali yake iliendelea vizuri hadi usiku huu wa January 27 hali yake ilipobadilika na kufariki dunia.
Wiki chache nyuma ilisemekana Mc D alikua akiendelea vizuri kwani hatua ngumu ya dozi ya kali ya kifua kikuuu alikua kashaivuka na sasa alikua amebadilishiwa dawa,aliongea kwa matumaini makubwa kuwa atarejea jukwaani muda si mrefu.
Miongoni mwa bendi alizozitumikia Mcd enzi ya uhai wake ni pamoja na Diamond Sound,Mashujaa Band na Twanga pepeta.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako