Majeshi ya Lebanon yametangaza kuwa kamanda wa cheo
cha juu wa kundi la kigaidi la Al Qaeda katika nchi hiyo Majid Al -
Majid amekufa akiwa kizuizini.
Kamanda huyo ambaye ni raia wa Saudi Arabia,
alikuwa ni kiongozi wa kundi la Abdulha Azzam ambalo lina uhusinao na
kundi la kigaidi la Al Qaeda, na ambalo pia limekuwa likikiri kuendesha
mashambulizi ya kigaidi na milipuko ya mabomu kulenga maeneo
yanayokaliwa na waumini wa madhehebu ya Shia katika siku za hivi
karibuni.
Miongoni mwa mashambulizi waliyokiri kuhusika nayo ni shambulizi katika Ubalozi wa Iran nchini Lebanon.
Maafisa wa jeshi wanasema Bwana Al Majid amekufa kutokana na maradhi ya figo na kwamba hali yake ilikuwa imezorota.
Al Majid alikamatwa mwezi uliopita na alikuwa akishikiliwa katika kizuizi cha siri.
-BBC

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako