Jumla
ya watu 27 wamepoteza maisha yao na wengine 27 wamejeruhiwa katika
matukio yanayohusisha ajali za treni zilizotokea nchini mwaka jana.
Kamanda
wa Kikosi cha Reli Tanzania, Saada Haji akizungumzia Mwananchi alisema
kwamba jumla ya ajali 79 zinazohusisha treni zilitokea mwaka jana katika
mikoa tofauti nchini.
Alisema
kuwa hata hivyo ajali nyingi kati ya hizo zimetokana na uzembe, ikiwemo
kulewa na kukaa juu ya reli, kuweka ‘headphone’ na kutembea relini na
madereva wa magari kukosa umakini wa kufuatilia alama za barabarani kwa
kuendesha mwendo kati hata mahali penye kivuko cha treni.
“
Treni linalofanya safari zake ndani ya jiji ndiyo ambalo kwa sasa
linahisisha vifo vya watu wengi kwa muda mfupi tangu kuanza kwa safari
zake watu 8 wamekufa huku wengine wakijeruhiwa,” alisema Kamanda Haji.
Alisisitiza”
Hasa katika eneo la Daraja la Buguruni kwa Mnyamani ndiyo eneo ambalo
ni hatari, kwani limekuwa na matukio ya ajali, wananchi wengi hujisahau
hukatiza juu ya reli kwa kuwa treni huwa halina breki za papo kwa papo
basi vifo au majeraha makubwa yanayowasababishia ulemavu wa kudumu,”
Akizungumzia
kuhusu matukio 285 ya uhalifu alisema kuwa yalitokea katika mikoa ya
Morogoro, Dodoma, Itigi, Tabora, Mwanza, Kigoma, Mpanda na Dar es
Salaam, ambayo yaliyokea katika maeneo ya reli na ndani ya treli.
“
Polisi wa kikosi hiki wamekuwa wakipambana kikamilifu, kuna siku
walifanikiwa kukamata mabegi yaliyowekea bangi, ambapo mtuhumiwa
alifikishwa mahakamani ", alisema.
Alisema kuwa Polisi hao pia waliwahi kumbaini mhalifu mmoja aliyekuwa na amebeba silaha isivyo halali ndani ya treni ambaye alikurupuka na kuitelekeza siraha hiyo
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako