Mwanza.Raia wa China ambaye ni meneja
uzalishaji katika kampuni ya ujenzi Shen Hai,46, amepandishwa kizimbani
kwa kosa la kuchana noti ya shilingi 10,000 ambayo ni mali ya Serikali
ya Tanzania.
Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi
wa mkoa Janeth Masesa, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Castus
Ndamugobas alidai kuwa Mchina huyo alitenda kosa hilo mnamo Desemba 3
mwaka jana katika maeneo ya uwanja wa ndege Wilaya ya Ilemela majira ya
saa 10:30 jioni ambapo kwa makusudi aliichana noti hiyo yenye namba
AY3748043, ambayo thamani yake ni Sh10,000 mali ya Serikali ya
Tanzania.
Mshtakiwa huyo ambaye ni meneja mzalishaji
aliyeajiriwa na Serikali ya Tanzania ili kufanya ukarabati katika Uwanja
wa Ndege wa Mwanza, alikana mashtaka yote na alirudishwa rumande baada
ya kutokidhi masharti ya dhamana na hakimu Masesa aliahirisha kesi hiyo
hadi Januari 8 mwaka huu ambapo itafikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya
kutajwa tena.
Kitendo hicho cha raia huyo wa China kuchana noti kilionyesha dharau kwa nchi ya Tanzania na raia wake.CHANZO MWANAINCHI
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako