Naibu
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt. Mahongoro Mahanga
akitoka katika chumba cha mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na
Upatanishi wiki iliyopita siku ya Jumanne baada ya kusomewa mashtaka
yake ya kumfanyisha kazi PS wake (Private Secretary) Bi. Itika Kasambala
katika ofisi yake ya Bunge kwa muda wa miaka kumi bila mkataba na
kusitisha kazi yake na kisha kulipa mafao ya laki mbili tu.
.Msaidizi wake wa ofisi ya Bunge afanya kazi miaka kumi chini yake bila mkataba
.Baada ya miaka kumi amlipa mafao ya laki mbili tu.
.Dada alalama kwamba Naibu Waziri alimtaka kimapenzi akakataa
Na. Mwandishi wetu
NAIBU
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Makongoro Mahanga
ameingia kwenye kashfa nzito ya kuvunja sheria za kazi nchini kwa
kumfanyisha kazi msaidizi wake (PS) wa ofisi yake Bunge kwa miaka kumi
bila mkataba na kumlipa fedha taslimu shilingi laki mbili tu (200,000)
kama mafao.
Naibu
Waziri, Mahanga anakuwa kiongozi wa kwanza kuingia kwenye kashfa akiwa
madarakani tena kwenye swala la ajira wakati yeye mwenyewe ni waziri
mwenye dhamana na maswala ya ajira na haki za wafanyakazi nchini chanzo
chetu kimeelezwa.
Naibu
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana akishuka katika ngazi za
mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi wiki iliyopita siku
ya Jumanne jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa sheria kazi na mahusiano kazini, Naibu Waziri amekiuka kifungu
cha 3 cha sheria ya Taasisi za kazi za mwaka 2004 na pia amekiuka
sehemu ya tatu ya viwango vya ajira na sehemu ndogo A kwa kushidwa
kuandika mkataba kwa mujibu wa kifungu cha 14 ibara ya kwanza kama
sheria ya kazi na mahusiano kazini inavyotaka.
Katika
kifungu hicho cha 14 ibara ya kwanza kinasema mkataba utakuwa wa
kipindi cha muda usiotajwa, mkataba wa kazi maalumu na mkataba unatakiwa
kuwa wa maandishi ambapo vyote Mhe Naibu Waziri hakufanya.
Picha
juu na chini ni baadhi ya nakala za malada ya kesi hiyo
iliyofunguliwa mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi na Bi.
Itika Kasambala dhidi ya Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya
Vijana.
Ibara
ya 15 kifungu cha.-(1) kinasema kwa kuzingatia masharti ya kifungu
kidogo cha (2) cha kifungu cha 19, mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi,
wakati mfanyakazi anapoanza kazi, taarifa zifuatazo kwa maandishi, jina,
umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi; mahali alipoajiriwa;
kazi zake; tarehe ya kuanza; muundo na muda wa mkataba; kituo cha kazi;
masaa ya kazi; ujira na njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao
mengine.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Bi.
Itika Kasambala (31) anasema alianza kazi kwa Mbunge huyo wa Segerea na
Naibu Waziri wa kazi Dkt. Mahanga, mwaka 2003 kama PS (Personal
Secretary) kwa makubaliano ya kumpa mshahara wa shilingi 120,000 kwa
mwezi lakini alianza kumlipa shilingi 50,000 tu.
“aliniambia
kwamba nianze kazi kwanza baadaye atanipa mkataba wa ajira na kunilipa
mafao ya hifadhi ya jamii na matibabu lakini baada ya miaka kumi
ananitumia sms akiwa Dodoma kwamba kazi basi sikuhitaji tena,” Kasambala
alisema.
Amesema
kwamba Mbunge huyo alimtumia sms akiwa kwenye vikao vya bunge mjini
dodoma mwaka jana mwezi wa sita akimjulisha kwamba ajira yake imeshafika
kikomo kwa sababu hana uwezo tena wa kumlipa mshahara na mahitaji
mengine ya kiofisi.
Kasambala
aliendelea kusema kwamba mara ya kwanza wakati anaanza kazi mwezi wa
tano mwaka 2003 baada ya msaidizi wa ofisi ya mbunge Mahanga kuacha kazi
na ndipo alipotafutwa yeye na walikwenda kuelewana kwa malipo ya
120,000 kwa mwezi.
Alisisitiza
kwamba mara baada ya kuanza kazi kwa ofisi ya mbunge alikuwa analipa
pesa kupitia mkononi na baadaye tigo pesa na baada ya muda akawa
anachukua pesa yake ya mshahara toka katika manisapaa ya Ilala kama
posho ya Mhe Mahanga kama diwani kila mwezi.
Dada
huyo kwa mshangao baada ya mahojiano ya muda mrefu alikiri kwamba Mhe
Mahanga alikuwa na nia ya dhati kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na
kumtaka aende Dodoma lakini alikataa kufanya masharti hayo.
“mwaka
juzi baada ya kuonyesha nia ya kunitaka kimapenzi alinipigia simu
akitaka niende Dodoma bungeni kwa mazungumzo zaidi kama msaidizi wake
lakini nilikataa,’ aliongeza Kasambala.
Amesema
tangu aanze kazi kwa Mhe Mahanga hakuwa anatoa huduma zozote kama
matibabu au fedha kwa ajili ya sikukuu ilikuwa ni mshahara tu wa 120,000
kwa mwezi lakini kila akimfuata ili waandikishiane mkataba alikuwa
akizungumsha bila sababu za msingi.
Bi
Kasambala aliongeza kuwa amefanya kazi Mhe Mahanga tangu akiwa mbunge wa
Ukonga na baadaye Segerea lakini ameshidwa kuheshimu sheria za ajira na
taratibu za kazi wakati yeye mwenyewe ni waziri mwenye dhamana ya ajira
kwa watanzania.
Amesema
mwaka jana tarehe 14/09/2013 alimtumia kwa Tigopesa kiasi cha shilingi
za Tanzania 200,000 kama mafao yake baada ya kufanya kazi kwa takribani
miaka 10 kama Msaidizi wake wa Ofisi ya Mbunge.
Bi. Itika Kasambala akiwa katika moja ya vyumba vya habari baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi.
Amesema
kwamba aliamua kwenda Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Mahoteli,
Majumbani na Kazi Nyingine (CHODAWU) kwa msaada wa ksiheria ba baada ya
kukutanishwa bado Mhe Mahanga akawa mgumu kukubaliana kiungwana mpaka
ikawalazimu kwenda mahakani Tume ya Usuluhishi na Upatanishi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi wakili wa Kasambala, Nyaisa Godwin alisema
kuwa kesi imefunguliwa mahakama ya kazi wiki iliyopita siku ya Jumanne,
Tume ya Usuluhishi na Upatanishi kesi namba CMA/DSM/ILA/R.711/13.
Wakili
Nyaisa alisisitiza kwamba Naibu Waziri aliiambia mahakama kwamba Dada
Kasambala alikuja kufanya kazi kwake kama mwanafunzi wa chuo kwenye
mazoezi lakini alishidwa kuithibitishia mahakama kwa ushawishi wa barua
ya (field to chuoni).
“tulishagazwa
na majibu ya waziri kwamba dada huyo alikuwa field, na nilimuuliza
field ya miaka kumi? Alishidwa kutoa jibu mbele ya mpatanishi
(Arbitrator),” amesema Nyaisa.
Bi.
Itika kasambala akiwa katika picha tofauti jijini Dar es Salaam baada ya
kuelezea sakata lake na Naibu Waziri wa kazi, Ajira na Maendeleo ya
Vijana.
Nyaisa
aliendelea kusema kutokana na matatizo ya kuachishwa kazi ghafla bila
taratibu dada huyo amepata maradhi ya presha, vidondo vya tumbo na
maradhi mengine baada ya kufanya kazi kwa Mhe Mbunge kwa miaka kumi bila
matibabu wala kulipiwa mifuko ya hifadhi za jamii.
Wakili
Nyaisa aliongeza kwamba kesi hiyo ya aina yake dhidi ya Naibu Waziri wa
Kazi itasomwa tena tarehe 13/02/2014 katika Tume ya Usuluhisho na
Upatanishi.
Juhudi
za kumtafuta, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt.
Mahanga hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya kiganjani kushidwa
kupatikana kwa muda mrefu alipotafutwa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako