Maelfu ya watu kutoka ndani ya jiji la Dar es salaam na viunga vyake walikusanyika hapo jana katika ibada kubwa ya matendo makuu ya Mungu iliyoambatana na tamasha kubwa la uimbaji katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam ambako ndiko makao makuu ya kanisa kubwa la Ufufuo na Uzima lililo chini ya askofu Josephat Gwajima.
Moja kati ya matukio yaliyomrudishia utukufu Mungu ni
pamoja na watu zaidi ya 1,000 waliompa Yesu maisha yao, mwanadada ambaye alikuwa akitembelea magongo kwa muda mrefu baada ya kugongwa na pikipiki hapo jana aliweza kutembea kwa mara nyingine pamoja na watu wengine waliokuwa wakitembelea magongo Mungu kuwaponya.
Pamoja na mengine moja ya ushuhuda uliovutia wengi ni wa binti Maria Togolani ambaye awali aliwahi kuchukuliwa msukule kisha kurudishwa kwa maombi kupitia kanisa hilo alizungumza kwa mara nyingine ushuhuda huo ambao ulitukia miaka takribani minne iliyopita ambapo alikaliliwa akisema huko msukuleni alikuwa pamoja na aliyekuwa mtangazaji kisha mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia viti maalumu marehemu Amina Chifupa wa Mpakanjia. Alipotoa ushuhuda huo kwa mara ya kwanza miaka hiyo ilimfanya mama wa marehemu Amina kufika kanisani hapo kumuona mchungaji Gwajima ili mwanae arudishwe kwakuwa siku alipokuwa anakufa alikuwa anatamka maneno ambayo mama huyo aliamini kuwa mwanae hakufa katika hali ya kawaida.
Kama haitoshi pia baba wa marehemu Amina mzee Chifupa aliwahi kufika kanisani hapo akiongozana na mkewe ili kuzungumza na mchungaji Gwajima kuhusu suala hilo ambalo baadhi ya vyombo vya habari viliwahi kukaririwa vikisema mchungaji Gwajima anamrudisha Amina Chifupa jambo ambalo hata hivyo halikutoka kwa mchungaji huyo bali binti huyo kumuona marehemu Amina Chifupa huko alikokuwa kama msukule, ambapo mchungaji Gwajima alikuwa tayari pamoja na waombaji wa kanisa hilo kumuomba Mungu ili Amina kurudi, hata hivyo zoezi hilo halikutimia kutokana na kutojulikana nini kilijili kwenye mazungumzo yake na wazazi wa binti huyo.
Binti Maria akitoa ushuhuda wake kwa mara nyingine kanisani hapo jana.
Ibada hiyo ilipambwa na sifa kutoka kwa waimbaji kama Flora Mbasha na mumewe Emanuel Mbasha, Maximilian Machumu a.k.a Mwana mapinduzi, na waimbaji wengine kutoka kanisa hilo ambalo limesheheni waimbaji ambao wamekuwa wakisaidiwa kupiga hatua kwenye uimbaji wao.
Flora Mbasha akimsifu Mungu ibadani hapo.
Watu waliopita mbele kumpa Kristo maisha yao.
Dada aliyeweza kutembea kwa mara nyingine.