Kufuatia
mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Dodoma, nyumba 127
zimebomolewa na mafuriko ambapo watu 493 wamekosa makazi ya kuishi, pia
nyumba 240 zimezingirwa na maji katika Kijiji cha Chipogolo Kata ya
Chipogolo tarafa ya Rudi Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma na kusababisha
jumla ya wakazi 1390 kukosa makazi ya kuishi.
Naibu
Waziri wa Nishati na madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe
Wilayani Mpwapwa Mh. George Boniface SimbaChawene amesema katika kikao
cha tathmini kilichofanyika mara baada ya kukagua eneo lililoathilika na
mafuriko, wamekubaliana hatua mbalimbali zichukuliwe ikiwemo kujenga
upya madaraja yaliyopo pamoja na kuongeza kimo na urefu wa madaraja hayo
kwa kuwa madaraja yaliyopo ni mafupi na yanazidiwa na maji.
a
Pia
Mbunge huyo ameiomba kamati ya maafa kufanya kila liwezekanalo
kuhakikisha kwamba wakazi wa kijiji hicho wanapata huduma mbalimbali
zikiwemo za Afya kwa kuwapa madawa, elimu pamoja na kuwaongezea
wataalamu wa afya, kuwapatia Mahema, mablaketi na magodoro na chakula.
Hii-ni-moja-kati-ya-nyumba-za-polisi-ambazo-zimeharibiwa-na-mafuriko |
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mh. Christopher Ryoba Kangoye
amewaomba wakazi wa kijiji hicho kuendelea kuwa wavumilivu katika
kipindi hiki kigumu wakati serikali kupitia kamati ya maafa Mkoa wa
Dodoma ikiendelea kushughulikias matatizo yao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David
A. Misime amewataadharisha wakazi wa kijiji hicho kuwa watulivu kwani
matatizo kama haya hayatatuliwi kwa vurugu badala yake watumie vikao
vinavyostahili kutatua matatizo yao “matatizo kama haya hayatatuliwi kwa kufanya fujo na kufunga barabara”
Wakati
huohuo Kituo cha Polisi Kata ya Chipogolo na nyumba tano za Askari wa
kituo hicho zimeanguka kutokana na mafuriko hayo, Kamanda Misime ametoa
pole kwa Askari wa kituo hicho na kuwasisitiza waendelee kufanya kazi
kwa maadili ya Jeshi bila kujali wakati tatizo lao linashughulikiwa na
mamlaka husika kwani vituo vya Polisi kama hivyo vipo chini ya
Mkurugenzi na wananchi kwakuwa vilijengwa kwa nguvu zao.
Kamisha-msaidizi-mwandamizi-wa-Polisi-Daid-Misime-akiongea-na-wakazi-wa-kijiji-cha-Chipogolo-namna-ya-kuweka-ulinzi-kijijini-hapo |
Kituo-cha-Polisi-Chipogolo-kilichobomolewa-na-mafuriko-hayo |
mafuriko-yaliharibu-vitu-mbalimbali |
Naibu-waziri-wa-Nishati-na-Madini-George-B.-Simbachawene-MB-akizungumza-na-wakazi-wa-Kijiji-hicho |
nyuma-ya-Askari-polisi-iliyobomolewa-na-maji |
SGT-SOTELI-wa-jeshi-la-polisi-kituo-cha-polisi-Chipogolo-ambaye-pia-ni-muathirika-wa-Mafuriko-hayo-akifafanua-jambo-kwa-Kamanda |
Hili-ni-eneo-lililokumbwa-na-mafuriko-hayo |
Hii-ni-moja-kati-ya-nyumba-za-polisi-ambazo-zimeharibiwa-na-mafuriko |