Jengo la pili kwa urefu New York City linalojulikana kwa jina la
Empire State Building likiwaka taa zenye rangi ya bendera ya South
Africa. Unaweza kuelewa kuwa ni jinsi gani dunia kwa ujumla imeguswa na
kifo cha kiongozi huyo aliekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya
ubaguzi wa rangi duniani.
Hapa ni makao makuu ya Umoja wa Mataifa Duniani New York City nako bendera inapepea nusu mlingoti kama unavyoona.
Apollo ni sehemu maarufu sana hapa New York City sehemu hii inapatika
125th Street Up town Harlem. Apollo ni maarufu sana kwani ndiyo
chimbuko la masuper star wote wa Marekani bila kupitia hapa na kupata
mzimu kwa kugusa mti maalum unaopatika ndani ya jengo hili basi uwezi
kuwa super star. Kila jumatano kunakuwa na mashindani ya kumpata super
star mpya kwa jina la (Amateur Night). Apollo wanatambua mchango wa
Mandela na kama unavyoona jina lake lina shine juu ya ubao wao wa
matangazo kama njia ya kumuenzi kiongozi huyo wa Africa.
Mishumaa inawaka na picha ya Mandela ikiwa juu na chini watu wakisign
na kuweka michumaa pamoja na maua. Hapa ni Apollo karibu na mlango
wakuingilia ndani ya jengo hili.
credit : vijimambo blog
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako